DAR ES SALAAM

NA MWANDISHI WETU

Mfanyabiashara, Jabir Kigoda, anakabiliwa
na tuhuma za kukutwa na magari matatu
yanayodaiwa kuwa ni ya wizi.
Magari hayo ya kifahari yamo kwenye
orodha ya magari yaliyoibwa nchini Afrika
Kusini.
JAMHURI limeambiwa kuwa Shirikisho la
Polisi wa Kimataifa (Interpol), tayari
limejulishwa kuhusu tukio hilo.

Magari hayo yamekamatwa nyumbani kwa
mtuhumiwa, Upanga jijini Dar es Salaam.
Nayo ni BMW X6 lenye namba za usajili T
270 CFP, Toyota Fortuner (T 239 DDA) na
Range Rover Sports ambayo namba zake
hazikupatikana mara moja. Yamehifadhiwa
katika Kituo Kikuu cha Polisi, Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam.
Jalada la shauri hilo limepewa namba
CD/IR/1966/2018. Mpelelezi wake ni Sajini
Stephano.
Taarifa kutoka Polisi zinasema Jabir
alikamatwa na kuwekwa rumande kwa siku
kadhaa kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
Wizi wa magari nchini Afrika Kusini uko
katika kiwango cha juu. Aprili 2016 hadi
Machi, mwaka jana magari 16,717 yaliibwa.
Kiwango hicho kilikuwa ni ongezeko la
asilimia 14 cha magari yaliyoibwa mwaka
mmoja kabla ya kipindi hicho.
Magari kadhaa yanayoibwa huuzwa katika
nchi mbalimbali zilizo Kusini mwa Jangwa la
Sahara; na Tanzania ikitajwa kuwa ‘pepo’
ya biashara hiyo kabla ya Serikali kuingilia
kati kuipunguza.
Jabir amezungumza na JAMHURI kuhusu
tuhuma hizo, lakini amekataa kutoa
ushirikiano, akidai kuwa Polisi ndio

wanaopaswa kulizungumzia suala hilo.
“Mimi siwezi kuzungumza, kama
umeambiwa lipo Polisi, basi zungumza nao
wewe wakueleze,

” amesema na kukata

simu.
Baadaye simu ilipopigwa, ilipokewa na mtu
mwenye sauti ya kike aliyejitambulisha
kuwa ni dada yake Jabir, lakini hakutaka
kutaja jina lake.
“Mimi ni dadake Jabir, kama hayo mambo
unayo ni vizuri mkawauliza Polisi wenyewe
badala ya kumuuliza kaka yangu,

amesema.
Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya
Kipolisi ya Dar es Salaam, Camillius
Wambura, amezungumza na JAMHURI kwa
simu, lakini amekataa kuingia kwenye
undani wa suala hilo.
“Mimi ni Mkuu wa Upelelezi wa Kanda
Maalumu, lakini yupo msemaji wa Jeshi la
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
ambaye sisi tukiandaa taarifa
tunampelekea. Muulize yeye maana mimi si
msemaji,

” amesema.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro
Mambosasa, amesema: “Wapo wasaidizi

wangu wanaofanya kazi za kupokea taarifa,
kuchunguza na kufikisha taarifa kwangu.
Hilo unaloniambia kwa kweli halijaletwa
kwangu. Sina taarifa zozote za kukupatia.”
Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Joseph
Solomon, ameliambia JAMHURI: “Msemaji
ni DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai). Mimi si msemaji, naomba
umuulize yeye.”
DCI Robert Boaz, amesema hawezi
kulisemea suala hilo moja kwa moja bila
kuingia kwenye mfumo ili kujua kama kweli
magari hayo yalikuwa yanatafutwa.
Amesema anajiepusha kusema kama
magari hayo ni ya wizi hadi hapo
atakapokuwa amepata taarifa na rekodi
sahihi.

…tamati….

Please follow and like us:
Pin Share