Taifa letu tangu Uhuru 1961 limekuwa likipitia katika nyakati tofauti za kiuchumi na kijamii hii ni kutokana na mifumo na mabadiliko ya siasa za dunia.
Kati ya mwaka 1867 hadi miaka 1985 taifa likiwa na sera ya uchumi dola yaani centralized economy hii sera ilipata misukosuko kutokana na uchumi wa dunia hasa mashirika ya kifedha ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani yaani WB NA IMF.
Kuanzia 1986 baada ya sera ya kiliberali kuanza maarufu kama ruksa hii ilibadili uelekeo wa uchumi kutoka uchumi dola na kuwa uchumi wa kiliberali yaani Free Economy System. Huu ni wakati ambapo wananchi wengi wakaanza kupata ladha ya kuwa na uchumi huru kama kumiliki viwanda, makampuni binafsi, taasisi za elimu ya juu.
Ikumbukwe katika mfumo wa uchumi viwanda na nyenzo zote za uzalishaji zilikuwa zinamilikiwa na kuendeshwa na Serikali mfano viwanda kama vile Urafiki Textile kilichopo Ubungo Dar es Salaam, MWATEX huko Mwanza, MUTEX huko Musoma, Mtibwa Sugar huko Morogoro. Awamu zote za uongozi zimekuwa na mchango mkubwa kwa taifa letu la Tanzania chini ya mwasisi baba yetu Hayati Julius Kambarage Nyerere.
BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE 1961 HADI 1985

Alipigania Uhuru wa Taifa letu, Aliunganisha taifa kwa lugha moja ya Kiswahili, Aliasisi Muungano wetu 1964.Aliasisi Sera ya Ujamaa na Kujitegemea katika Azimiao la Arusha 1967, alianziasha uchumi dola yaani Centralized Economy hii ilikuwa ni kuweka mazingira ya kujitegemea kama taifa huru.
Aliunganisha makabila yote nakuwa taifa moja lenye umoja na mshikamano. Alishajihisha kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi 1992.Kwa kutoa hoja ya kifalsafa kuwa CCM ikubali vyama vingi wakati ambapo watu wengi hawa itaji kuwa na vyama vingi. Aliongoza vita dhidi ya adui mvamizi nduli amini dada na kulinda mipaka ya nchi.
Alitaifisha shule za binafsi ili ziweze toa fursa ya elimu kwa wote bila kujari dhehebu au dini hii ilikuwa ni kuleta usawa wa elimu. Alianzisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kupata watalaam wa kuongoza taifa. Aliondoa mfumo wa uongozi wa kijadi kingship au chief Dom hii ilikuwa na shabaha ya kujenga umoja na mshikamano.
Kuna mengi mazuri ambayo baba wa Taifa ameyatekeleza na kuwa historia isiyostahaulika na ambayo hadi leo tunaendelea kuyafuata na kuyasimamia katika nyanja mbalimbali.
AWAMU YA PILI MCHANGO WA HAYATI ALI HASSANI MWINYI 1985 HADI 1995

Alianzisha Uchumi wa Kiliberali ikifahamika kama ruksa, aliaasisi sekta binafsi ikiwemo taasisis za elimu ya juu.
Aliasisi vyama vingi vya siasa hasa kwa kuunda tume ya Jaji Francis Nyarali iliyoleta maoni yaw ananchi juu ya vyama vingi. Aliimarisha diplpomasia ya kima Taifa ,tukishuhudia ujio wa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa John mwaka 1990.
Chini ya uongozi hayati Mwinyi Tanzania ilipata maendeleo makubwa yaliyotokana na juhudi zake ambazo mpaka sasa tunaendelea kujivunia kutokana na uongozi wake ambao umekuwa mfano bora katika kikazi na kikazi.
AWAMU YA TATU MCHANGO WA HAYATI BENJAMINI WILIAM MKAPA 1995 HADI 2005

Alichagiza sera ya ubinafsishaji, Aliichagiza utandawazi, Aliaendeleza sera ya uwazi na ukweli, Alijenga miundombinu ya Barabara na madaraja ikiwemo Daraja la mkapa, Alipunguza deni la taifa na kuongeza uwezo wa kujitegemea kama taifa, Alishiriki uhuishwaji wa Jumuiya ya Africa Mashariki 1999 hadi 2000.
Alijenga majengo ya Benki Kuu na kuanzisha TRA, Alianzisha Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Alianzisha programu za kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa jamii ikiwemo MKUKUTA, MKURABITA, Na MKUZA, Alijenga jengo la Bunge Dodoma na uwanja wa Taifa.
Kutokana na juhudi zake za kuchochea maendeleo ya Tanzania, hadi sasa bado mchango wake wa kuipeleka Tanzania kwenye uchumi mkubwa zaidi zinaendelea kutekelezwa kwa kuhakikisha wananchi wanafaidika na matunda ya nchi yao. Mengi aliyafanya na hadi sasa yanatekelezwa ili kufikia ndoto alizotamani nchi kuwa na maendeleo.
AWAMU YA NNE YA MHESHIMWA JAKAYA MRISHO KIKWETE

Mchango wake katika Uchumi wa taifa
Aliunganisha mikoa yote kwa Barabara ya lami hii imekuwa kichocheo kikubwa cha Uchumi kupitia sekata ya usafirishaji ikiundwa TANROAD na TARURA kama mamlaka za usimamizi wa miundombinu ya barabarani.
Amejenga shule za sekondari kila kata nchi nzima hii ime chochea Uchumi na hata watu wengi kuwa na fursa ya kupata elimu kwa mazingira mahalia, amejenga taasisi za afya hospitali za kibingwa na huduma za kibigwa bobezi ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Hospitali ya Mloganzila na Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma.
Alihamasisha upimaji wa Afya ili kulinda afya ya jamii na kujepusha na magonjwa akiongoza zoezi la kupima HIV hii ina dhihirisha jinsi alivyo kuwa kiongozi mathubuti, Alijenga vyuo vikuu kikiwemo chuo kikuu cha Dodoma
Alianzisha mikoa mipya ikiwemo mkoa wa Njombe, Songwe, Simiyu shabaha kuu ni kusogeza huduma za kiserikali karibu na wananchi, Aliboresha mfumo wa demokrasia kwa kuhakikisha vyama vya siasa vinafanyakazi kwa mujibu wa sheria.
Alirahisisha na kutoa ajira kwa vijana hasa za ualimu bila ya usaili, Aliimarisha diplomasia ya kiuchumi, kikanda na kimataifa hata kuwezesha aliyekuwa Rais wa Marekani kutembelea Tanzania Barack Hussein Obama.
AWAMU YA TANO 2015 2021 HAYATI DK JOHN MAGUFULI

Alibuni na kuanzsha miradi ya kimkakati yenye shabaha ya kukuza Uchumi ikiwemo Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere, SGR,Alianzisha Mahakama ya Kushughurika na Kesi za Uhujumu Uchumi ilisaidia kuthibiti vitendo vya rushwa na ubadhilifu.
Alishajihisha wajasiriamali wadogo kufanya biashara kwa uhuru kila mahali kwa kutumia kitambulisho cha machinga kwa sh 20,000 kwa mwaka, Alihamasisha wananchi kujitegemea hasa wakati wa kupambana na janga la UVIKO 19.
Allifufua Shirika la Ndege ATCL kwa kununua ndege mpy, alifufua reli ya kaskazini, aliboresha huduma za afya kwa kununua vifaa tiba vya kisasa na kujenga hospitali za kanda ikiwemo hospitali ya kanda ya Chato, Mtwara na kuboreha huduma katika hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya afya nchi nzima, alifanikisha kuhamishia serikali Dodoma na kujenga mji wa serikali yaani Magufuli City, Alibana matumizi hasa kwa kutosafari hasa nje ya Bara la Africa.
AWAMU YA SITA CHINI YA DK SAMIA SULUHU HASSAN

DK Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Awamu ya Sita aliapishwa kushika madaraka baada ya kifo cha Rais John Magufuli hivyo mpaka 2025 amechaguliwa kuendelea na awamu yake ya pili. Huyu bado anaeendelea kuiongoza nchi hivyo mchango wake kwa kipindi cha kwanza ni mkubwa ambapo amemalizia miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa katika awamu ya tano.
Amelinda na kudumisha muungano,ametoa mikopo isiyo na riba kwa wajasiria mali ili kuchochea uchumi, ameimarisha mifumo ya usafirishaji kwa sasa mabasi ya abiria yana safari usiku na mchana, amerejesha Bunge kuwa mubashara katika vikao vya Bunge, ameimarisha diplomasia ya kikanda na kimataifa, ameimarisha ujenzi wa miundombinu ya barabara, shule za msingi na sekondari, ameimarisha upatikanaji wa nishati safi ambapo upatikanaji wa umeme umekuwa wa uhakika.
Bado ana mipango mingi ya kuhakikisha Tanzania jana inakuwa tofauti na Tanzania ya leo, kwa kuimarisha huduma mbalimbali katika hospitali, elimu na kuinua uchumi wa taifa.

Hitmisho
Kiuhalisia taifa letu nimiongoni mwa mataifa yanayo endelea na kila awamu tumeshuhudia ikiwa na mchango wake katika kuivusha nchi toka hatua moja hadi nyingine uhalisia ni kwamba maadui wa tatu amabao ni ujinga,umaskini na maradhi serikali katika kipindi chote imekuwa iki pambana na maadui hawa watatu kwa kuweka mazingira wezeshi ya kuwaondoa maadui hao.
Hivyo wananchi hatuna budi ya kuiunga mjkono serikali yetu kadri inayowezekana kwa sasa taifa letu lina barabara nzuri, umeme kila Kijiji,maji,hospitali za kiasasa, changamoto haziwezi kukosekana lakini kwa hatua hii
Taifa letu limeendelea na linazidi kuendelea. Pia haya mafanikio yote ya kuendelea kwa taifa letu kunatokana na utekelezaji wa ilani na miongozo ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Makala hii imeandaliwa na msomaji wetu ambaye ni;
JOHN FRANCIS HAULE
MKUU WA SOKO LA SAMUNGE
JIJINI ARUSHA
SM 0756 717 987 AU 0711993907


