Mkoa wa Arusha umekuwa mshindi wa tatu kwa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini vinavyofanya vizuri katika utoaji wa taarifa kwa umma miongoni mwa mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa mwaka 2023/2024.

Tuzo hizo zilitangazwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Thobias Mkoba, mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Kongamano la Wanahabari Tanzania na Kikao Kazi cha 19 cha Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, Juni 18, 2024 kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam na kutolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano naTeknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, wakati akifunga Kikao kazi mapema leo Juni 21, 2024.

Katika picha ni Afisa Habari Mkoa Wa Arusha Elinipa Lupembe akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Nape Nauye.