MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA MONDULI.


Julius Kalanga (Pichani) ametangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge katika Jimbo la Monduli mkoani Arusha kwa tiketi ya CCM, baada ya kupata kura 65, 714 dhidi ya kura 3,187 alizopata mshindani wake Yonas Leiser wa CHADEMA.
Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo Steven Ulaya ametaja matokeo ya wagombea wengine katika jimbo hilo kama ifuatavyo.

Elizabeth Michael wa Chama cha Wakulima – Kura 16.

Wilfred Mlay wa ACT Wazalendo – Kura 144.

Francis Ringo wa ADA-TADEA – Kura 21.

Omary Kaigo wa DP – Kura 34.

Simon Ngirisho wa Demokrasia Makini – Kura 35.

Feruzy Juma wa NRA – Kura 45

Please follow and like us:
Pin Share