Timu ya Kagera Sugar imezinduka na kupata ushindi wa kwanza wa msimu baada ya kuichapa Polisi Tanzania mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na kiungo Abdulaziz Makame dakika ya 10 na mshambuliaji Mbaraka Yussuf dakika ya 52.

Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi tano na kusogea nafasi ya 13, wakati Polisi inayobaki na pointi zake mbili baada ya wote kucheza mechi sita, sasa inachukua nafasi ya Ihefu mkiani mwa ligi.