Na Abel Paul, Abuja Nigeria

Kaimu Balozi, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Nigeria amewapongeza askari wa kike kutoka Tanzania waliofika Jijini Abuja Nchini Nigeria kushiriki mafunzo ambayo yalichukua siku Tano.

Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 5,2024 na Kaimu Balozi, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Nigeria, ambapo amewataka maafisa na askari pindi watakaporudi Nchini Tanzania kutumia mafunzo hayo vyema ili kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku.

Ameongeza kuwa mafunzo walioyapata yanakwenda kuongeza thamani ya utendaji wa kazi kwa askari na wasimamizi wa sheria.

Vilevile amewaomba askari hao pindi watakapofika Nchini Tanzania kuwafundisha wenzao na kuwapa elimu nzuri walioipata katika mafunzo yao Abuja.

Vilevile amewashukuru kwa namna walivyo itangaza vyema Nchi ya Tanzania katika sekta ya utalii na vivutio vingi vilivyopo Tanzania.