Idara Uhamiaji Mkoa wa Arusha usiku wa kuamkia tarehe 05/07/2024 imefanikiwa kukamata raia 28 wa Ethiopia maeneo ya Uwanja wa ndege wa kisongo uliopo nje kidogo ya jiji la Arusha, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama.

Idara ya Uhamiaji baada ya kuwakamata raia 28 wa Ethiopia. Kwa mujibu wa maelezo yao walikuwa wamepakiwa kwenye lori la mizigo ambalo lilipata ajali baada ya kugongana na gari lingine ndipo wakashuka na kujificha porini maeneo hayo.

Baada ya kupekuliwa baadhi ya raia hao walikutwa na majeraha kwenye miili yao haswa maeneo ya kichwani yaliyosababishwa na ajali hiyo.
Raia hao waliingia nchini kutokea Nchini Kenya kwa lengo la kwenda Afrika ya Kusini kupitia Tanzania, wote waliokamatwa waliingia nchini kinyume cha sheria kwa kuwa hawakuwa na pasipoti za Taifa lao.

Idara ya Uhamiaji inaendelea kutafuta gari lililotimika kusafisha raia hao pamoja na wasafirishaji.

Tunapenda kutoa wito kwa wananchi kutokujihusisha kwa namna yoyote ile na usafirishaji haramu ya binadamu na pindi watapobaini kwamba wapo raia wa kigeni wanaosafirishwa kimagendo watoe taarifa kwenye vyombo vya dora ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na pia tunaomba wanachi kutoa ushirikiano kwa Idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya usalama ili kukomesha vitendo vya Uhamiaji haramu.