Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki imemchagua Daniel Kalinaki wa Jukwaa la Wahariri Uganda kuwa Rais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki kuanzia Mei 12, 2023, ambapo ataongoza kwa mwaka mmoja.

Deodatus Balile, ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), naye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, kuanzia Mei, 2024 hadi Mei, 2025.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Balile anasubiri kushika wadhifa wa Urais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki mwezi Mei 2024, kwa sasa atakuwa ni Naibu Rais wa Jumuiya ya Wahariri ya Afrika Mashariki.

Umoja wa Wahariri wa Afrika Mashariki Katiba yake inatoa nafasi ya kumwandaa kiongozi wake ajaye kwa mwaka mmoja baada ya kumchagua kama sehemu ya maandalizi ya kuifahamu vyema kazi yake kabla ya kushika madaraka hayo rasmi.

By Jamhuri