Mahakama ya Rufaa nchini Ufaransa, imeshikilia kifungo cha miaka mitatu jela, dhidi ya rais wa zamani Nicolas Sarkozy kwa kosa la ufisadi na kushawishi kupewa taarifa kuhusu uchunguzi dhidi yake. 

Katika uamuzi wa mahakama hiyo ya rufa jijini Paris, kiongozi huyo wa zamani wa Ufaransa, anaweza tumikia kifungo chake nyumbani akiwa amevalia kitambulisho cha kuonyesha uamuzi huo.

Sarkozy alipewa kifungo cha miaka mitatu jela kwa makosa ya kujaribu kushawishi jaji kwenye kesi nyingine tofauti.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 68, alikuwa rais wa kwanza wa Ufaransa kutakiwa kufungwa jela.

Alihukumiwa kwa kujaribu kupata taarifa kuhusu kesi aliyokuwa anakabiliwa nayo mwaka wa 2014 baada yake kuondoka ofisini.

Inadaiwa kuwa baada yake kumaliza hatamu yake, alikata kupata taarifa kuhusu kesi yake na iwapo jaji angefanya hivyo, angepewa kazi yenye kiwango cha juu.

Rais huyo wa zamani pia alizuiwa kuwania katika nyadhifa yoyote ya umma kwa miaka mitatu.Hii ni mojawapo ya kesi anazokabiliwa nazo kiongozi huyo wa zamani wa Ufaransa, tuhuma ambazo hata hivyo amezikana zote.

Nicolas Sarkozy alihudumu kama rais kwa muhula mmoja mwaka wa 2007

By Jamhuri