Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Florent Kyombo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete wakimkabidhi fedha mlengwa wa TASAF Wilayani Uyui Amina Abdallah zilizochangwa na Wajumbe wa Kamati hiyo kumuwezesha mlengwa huyo kukamilisha ujenzi wa nyumba aliyoanza kuijenga kutokana na ruzuku ya TASAF anayoipata.
Mlengwa wa TASAF, wa Kata ya Magiri wilayani Uyui, mkoani Tabora, Amina Abdallah akipokea michango ya fedha kutoka kwa Jenista Mhagama na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria, vingozi na watendaji wa Serikali waliyomchangia kumuwezesha kukamilisha ujenzi wa nyumba aliyoianza kuijenga kutokana na ruzuku ya TASAF anayoipata.
Mlengwa wa TASAF wa Kata ya Magiri wilayani Uyui, mkoani Tabora Amina Abdallah akitoa neno la shukurani kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria, vingozi na watendaji wa Serikali baada ya kumpatia fedha kiasi cha shilingi 530,000 kumuwezesha kukamilisha ujenzi wa nyumba aliyoianza kuijenga kutokana na ruzuku ya TASAF anayoipata.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria kwa upendo waliouonyesha kwa mlengwa wa TASAF, katika Kata ya Migiri Wilayani Uyui Bi. Amina Abdallah kwa mchango wa kumuwezesha mlengwa huyo kukamilisha ujenzi wa nyumba aliyoanza kuijenga kutokana na ruzuku ya TASAF anayoipata.

By Jamhuri