Na Tatu Saad,JamhuriMedia
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Baraza la Michezo Tanzania ‘BMT’ linategemea kutoa tuzo kwa wana michezo mbalimbali Ijumaa Machi 17,2023.
Tuzo hizo zijilikanazo Kama National Sports Council Awards (NSCA) zitagawiwa katika ukumbi wa Mlimani City kwa wana michezo kutoka katika aina mbalimbali za michezo,waliofanya vizuri mwaka 2022.
Kama Serikali,imeona mchango wa wanamichezo katika michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu wa wanawake kwa wanaume, mpira wa kikapu, mpira wa gofu, sarakasi, Masumbwi na michezo mingine mingi
Kwa upande wa mpira wa miguu wana michezo wa soka hilo wamefanikiwa kuiinua ligi ya Tanzania na kuifanya ishike nafasi ya tano kwa ligi bora Afrika.
Kwa kuona hayo Serikali imeamua kutoa tuzo kwa wale wote waliofanya vizuri mwaka 2022 ili kuleta mitihani waendelee kufanya vizuri zaidi kwa faida ya Taifa la Tanzania.
Serikali imekuwa ikiwapa ushirikiano wana michezo kwa kuonesha wanajali uwepo wao na kazi zao kwa ujumla kwa kutoa tuzo hizi.
Hata hivyo sio tu wana michezo pia wasanii wa muziki na filamu nchini Tanzania huwa wanapewa tuzo ambazo zinazidi kuchochea ushindani mkubwa katika tasnia, kwa kuongeza juhudi na ufanisi mkubwa katika kazi zao.