Na Byarugaba Innocent, JamhuriMedia, Kibaha

Leo Jumatano Novemba 1,2023 Kamati ya Fedha na Utawala imefanya ziara kwenye kata tatu kuona utekelezaji wa Miradi mikubwa ya elimu na afya.

Miradi iliyotembelewa ni ijenzi wa shule ya msingi mpya kwenye Kata ya Kongowe kwa gharama ya Shilingi 475,300,000, ujenzi wa shule ya sekondari mpya na miundombinu yake lwenye Kata ya Mkuza iliyogharimu kiasi cha shilingi 528,998,425 pamoja na duka la dawa na chumba chenye mitambo ya huduma ya mionzi kwenye Kituo cha Afya Mkoani Kata ya Tumbi.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Fokasi Bundala amesema waheshimiwa madiwani wameridhishwa na utekelezaji wake na kwamba hiyo ni tafsiri ya ushirikiano kati ya wakandarasi na kamati za usimamizi.

Mwalimu Mkuu wa Shule Mama ya Kongowe Wamala Mussa amesema shule mpya itakuwa mkombozi kwenye eneo hilo kwani shule kongwe ina wanafunzi 1939 hivyo shule mpya itapunguza uwingi na msongamano madarasani na kutoa fursa kwa walimu kufundisha vema na wanafunzi kupokea masomo vizuri hali itakayoongeza ufaulu

Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalum Selina Wilsoni amesema kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuleta fedha za miradi Kibaha ni kubwa hivyo wazazi wanatakiwa kumuunga mkono kwa kuwafunda watoto wao waitunze miradi hiyo ili itumike kwa muda mrefu na vizazi vijavyo.

Kwa upande wa shule mpya ya Sekondari, Mbegu Kambi Legeza na Hamisi Shomari wametoa rai kwa walimu kuanza kuandika maombi ya kujengewa mabweni ili iwe ya bweni kwani jiographia yake sio rafiki kwa wanafunzi kutembea zaidi ya kilometa 8

Diwani wa Kata ya Tangini Mfalme Kabuga ameendelea kuungana na Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kwa kusisitiza agenda ya upandaji miti ili kutunza Mazingira na kutoa kivuli kwa wanafunzi wakati wa joto Kali huku Mbegu Kambi Legeza akitoa rai ya kupanda miti ya kivuli na Mlmatunda ambayo ni rafiki kwa miundombinu iliyojengwa.

Miradi ya Maendeleo kwa robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2023/2024 imekaguliwa na Kamati tatu Kamati ya Mipango Miji na Mazingira,Kamati ya Uchumi na huduma za Jamii na Kamati ya Fedha na Utawala