Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani tarehe 8 Machi 2024 wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group iliyopo TAZARA wilaya ya Temeke watatoa  huduma za tiba mkoba zijulikanazo  kwa  jina la Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya kambi maalumu ya  upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Upimaji huu ufanyika kwa watoto na watu wazima tarehe 02-03/03/2024 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili  jioni katika Hospitali ya JKCI Dar Group.

Aidha katika kambi hii kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na  kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0787941606 Dkt. Samwel  Rweyemamu , 0684345921 Flaviana Masegesa, 0783922571 Irene Mbonde  na 0674179036 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group.

 “Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.