Kanoute mchezaji bora Novemba

Kiungo wa Simba SC, Sadio Kanoute, ametwaa tuzo wa mchezaji bora wa Simba kwa mwezi Novemba baada ya kuwashinda beki Shomari Kapombe na kiungo Mzamiru Yasin kwa kura zilizopigwa na mashabiki wa timu hiyo. 

Kwa ushindi huo Sadio Kanoute atapata tuzo na pesa za kitanzania Milioni mbili (2,000,000/-) toka kwa wadhamini wa tuzo hizo, Emirates Aluminium,  kama sehemu ya zawadi baada ya ushindi