Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ameongoza Kikao Kazi na Viongozi wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu ambapo lengo la kikao hicho ni kuhakikisha taifa linakua salama, kuimarisha na kulinda wananchi juu ya kadhia hiyo ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu.

Kikao hicho kimefanyika Jijini Dodoma ambapo kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Gabriel Thobias Mwita akimwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Seperatus Fella na Viongozi wengine kutoka wizarani.

Waziri Katambi pia alikagua Kituo cha huduma ya mawasiliano cha kupokea taarifa na kutoa Elimu kuhusu madhara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Jijini Dodoma.