Na Mwandishi Wetu, JAMHURI MEDIA

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imesema bado haijakamilisha kuandaa hukumu katika  kesi inayowakabili Meneja wa Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma(PSSSF) Kanda ya Arusha,Rajabu Kinande na wenzake wanne

Washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la wizi wa vitu mbalimbali vya dukani vyenye thamani ya Sh. milioni 68.4

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo ,Fadhili Luvinga amesema hayo leo Ijumaa, Machi 27, 2023 kuwa washtakiwa hao wamekuja  kwa ajili ya kuwasomea  hukumu lakini mahakama hiyo  bado hajaikamilisha hukumu hiyo 

“Hukumu yenu sijaikamilisha nilikuwa na hukumu za kesi zingine nilikiwa naandaa hivyo nitapanga tarehe ya karibu kwa kuwa shtaka lenu ni la muda mrefu la mwaka 2021,”amesema Luvinga 

Soma: Kesi ya aliyekuwa kigogo wa PSSSF na wenzake yazidi kurindima

:Kesi ya aliyekuwa kigogo PSSSF na wenzake yaahirishwa tena

Awali wakili wa Serikali,Mosie Kaima ameieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya hukumu na wapo katika hatua ya kuikamilisha 

Mbali na Kinande washtakiwa wengine ni Ashura Kapera Farida Mbonaheri(34),Mohamed Miraji(48) na Msafiri Raha.

Katika kesi ya msingi kati ya Juni 16,2020 mtaa wa Gerezani wilaya ya Ilala washtakiwa wote kwa pamoja walivunja na kuingia kwenye duka la Mohamed Soli kwa nia ya kutenda wizi na waliiba vitu mbalimbali vikiwemo Vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya  Sh milioni 68.4 .

By Jamhuri