Na Aziza Nangwa,JamhuriMedia,Dar

Jaji Mwenegoha wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi ameamuru kesi ya mgogoro wa ardhi dhidi ya Frida Kysesi na Shaabani Kapelele ilirudi Baraza la Ardhi la Wilaya kwa ajili ya kusikilizwa.

Uamuzi huo ulifikiwa jana baada ya kupitia rufaa iliyokatwa kupinga shauri la ardhi kuanza kusikilizwa ngazi ya wilaya badala ya kuanzia ngazi ya kata.

Amesema Mahakama imepitia mwenendo wa Mheshimiwa Kirumbi, wa rufani walifikisha shauri Mahakamani baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa Mahakama ya chini uliotupilia mbali hoja zao za pingamizi.

“Maombi yanakinzana na kifungu 79(2) cha Sheria ya mashauri ya madai, kifungu kinakataza kukatia rufani uamuzi katika shauri lolote ambalo halijaisha.

“Maombi sio sahihi wa rufani wanatakiwa wasubiri hadi shauri liishe ndio walikatie rufani,” amesema.

Awali kesi hiyo ilikuwa Frida Kyesi alilalamika kupitia Gazeti la Jamhuri kutokuishi kwa amani kwenye eneo lake yeye pamoja na wanunuzi aliowauzia vipande katika mtaa wa Pugu Kinyamwezi, kwa kuvamiwa mara kwa mara na Shabani Kapelele pamoja na kundi lake kuwabomolea makazi yao kinyume cha sheria mpaka shauri hilo kufika mahakamani.

Mmoja wa majirani wa eneo hilo Rashidi Kirumbi amefafanua kwamba mama huyo anamfahamu muda mrefu tangu mwaka ya 1990, alikuwa akiishi na watoto wake kama mmikliki wa eneo hilo.

“Nakumbuka nikiwa ninasoma niko shule ya msingi miaka ya 90 mama huyo alikwenda kwa baba yangu mzazi na kumuomba amuuzie sehemu ya eneo letu,mzee alifanya hivyo akamuuzia kihalali hata seriakali ya kijiji na mtaa inamjua “amesema Kirumbi.

Kirumbi amesema eneo hilo ni la mama Frida tangu akiwa mdogo yuko shule ,kwa sababu baba yake alishiriki kumuuzia baadhi ya eneo lao katika sehemu ya ekali zake ishirini.

“Mimi nimezaliwa hapa mwaka 1961 nimesoma eneo hili na ninawajua watu wengi akiwemo mama Frida kama mama mjane,amekuwa akiwalea watoto wake kwa kutumia kipato cha kazi na bishara za kuku na zingine kwa kweli serikali ilione hilo imsadie mama huyo kupata haki yake”amesema Kirumbi.

Akizungumza na gazeti la Jamhuri kwa masikitiko Frida Kessy amesema alikwenda katika kijiji cha pugu kajiungeni mwaka 1982 na ilipofika mwaka 1986 alibahatika kununua eneo la shamba ekali 20 Pugu Kinyamwezi.

Amesema eneo hilo analimiliki kihahali na analipia kodi kwa miaka yote bila ya kuwa na shida ,mpaka ikafikia hatua ya kuligawa kwa kanisa .

Ilipofika Januari mwaka 2021 ndipo alipotokea kijana anaiyeitwa Shabani Kapelele na timu yake walivamia kiwanja namba 458 yenye ukubwa wa mraba 42054 kilichopo kata ya Pugu Mwakanga kitalu B

By Jamhuri