Mhariri Mtendaji Gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile akizungumza na Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis alipotembelea ofisi za gazeti hilo leo Machi 13, 2023.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi,tayari miradi 223 imesainiwa na kuvuka lengo la Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hayo yamebainishwa leo Machi 13,2023 na Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis wakati alipofanya ziara katika Kampuni Jamhuri Ltd linalochapisha Gazeti la Jamhuri.

Amesema kuwa,kuna mengi ya kujivunia tangu katika kipindi cha miaka miaka miwili chini ya Rais Mwinyi kwani ndani ya kipindi hicho kuna mengi yamefanyika na kuchangiza maendeleo Zanzibar.

Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis (kulia), akizungumza na Naibu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, Manyerere Jackton (kushoto) wakati alipotembelea ofisi za gazeti hilo leo Machi 13, 2023 Jijini Dar es Salaam.

“Kipindi cha miaka miwili miradi 223 imesainiwa na kuvuka malengo ambayo Serikali ilijiwekea na hata ukilinganisha na kipindi cha uongozi uliopita ambapo miradi 210 ilisainiwa kwa kipindi cha miaka 6 haya ni mafanikio makubwa na ya kujivunia,” amesema Khamis.

Kutokana na mafanikio hayo makubwa wanaamini kuwa kipindi cha kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 Rais Mwinyi hatokuwa na kazi ya kufanya kwani tayari aliyoahidi ametekeleza na amevuka malengo.

Khamis amesema kuwa bado kuna jitihada kubwa za kuibadili Zanzibarz inaendelea ikiwemo uboreshaji wa majengo ya hoteli na kitalii ili kuwa katika mazingira ya kuvutia.

Katika kuchagiza maendeleo Serikali imeboresha sekta ya afya kwa kujenga hospitali za wilaya,mikoa ambazo zitakuwa kubwa na zenye sifa kwa kupatikana kwa huduma mbalimbali.

Pia kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye mita 6 na urefu 275 ambazo kati ya hizo zitakuwa Mkoa wa Mjini na za mfano katika Afrika Mashariki.

Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis
Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis akisalimia na Mhariri Mtendaji Gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile alipotembelea ofisi za gazeti hilo leo Machi 13, 2023

By Jamhuri