Na Mwandishi Wetu JAMHURI MEDIA Dar Es Salaam

Serikali imesema kuwa mkutano wa Jukwaa la chakula Barani Afrika (AGRF) ni wa kimkakati kwa Tanzania ambapo mageuzi makubwa yanatarajiwa kushuhudiwa katika kilimo.

Mageuzi hayo ni pamoja na kufanya kilimo kuwa cha kisasa kwa njia ya umwagiliaji, matumizi ya mbegu bora, na hifadhi nzuri ya mazao, ambapo watanzania wanakwenda kuachana na kilimo cha mazoea kwa kutegemea mvua.

Akizungumzia juu ya Mkutano huo wa AGRF unaoendelea jijini Dar es Salaam Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema sasa watanzania watakwenda kunufaika baada ya miaka mingi ya kilimo kisicho kuwa na tija.

“Nafahamu uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na serikali yetu katika sekta ya Kilimo kwa miaka miwili mfululizo tumeendelea kuwa bajeti Trilioni 01 ambayo haikawahi kutokea kwa ajili ya kufanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya kilimo.” Amsema Msigwa

“kufanya mageuzi ya kuwatoa watanzania kwenye kilimo cha mazoea cha kutegemea mvua kwenda kwenye kilkmo cha umwagiliaji watumie mbegu bora, tuwe na hifadhi nzuri ya amazao lakini zaidi ya hapo tuwasaidie vijana kwenda kwenye kilimo cha ambapo wanapata manufaa makubwa badala ya kazi nyingi ambazo wamefanya na hazikuwa na tija kwa mda mrefu.” Amesema Msigwa

Katika kuelekea kwenye kilele cha mkutano huo ambao leo ni siku ya pili, kesho Alhamis Septemba 07, 2023 Msigwa ameeleza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan pamoja na Marais wengine wa mataifa zaidi ya saba, watahudhuria ambapo watapokea ripoti ya namna ambavyo vijana wa afrika wanajishughulisha na kilimo barani humo lakini pia kusoma maazimio ya mkutano huo.

” Rais Samia Suluhua Hassan Atakuwa na ule mkutano wa vijana azungumze nao atawahutubia lakini ye mwenyewe pia atapokea taarifa ya namna ambavyo vijana wa afrika wanajihusisha na kilimo na wanatumia fursa mbalimbali za kilimo na yeye atatoa hotuba yake ya namna ambavyo anaona ni mwelekeo sahihi wa bara letu la afrika kwa kusaidia eneo hili la vijana kupata ajira kupitia kilimo ” Amesema Msigwa

Mbali na hayo, Msigwa amesema kuwa kesho baada ya mkutano Rais Samia amewaalika wageni mbalimbali pamoja na Marais watakaohudhuria, chakula cha jioni katika Ikulu ya Dar es Salaam ambapo hafka hiyo itaambatana na utoaji wa tuzo ya mzalishaji bora wa chakula barani.

“Kesho hiyo jioni Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaalika wageni mbalimbali watakwenda ilikulu kwa chakula cha jioni ambako ndiko sasa itatolewa tuzo ya chakula Afrika.”

“Kwa hiyo ni tukio muhimu la kutambua mchango wa kuzalisha chakula kwenye bara letu la afrika kwa sababu moja ya changamoto tulizonazo ni upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo kwa hiyo tuzo ya mzalishaji wa chakula Afrika itatolewa kesho na kesho kutwa itakuwa siku ya ufungaji.”

Mkutano wa AGRF ni wa pili kufanyika nchini Tanzania ukiwakutanisha zaidi ya watu 3000 kutoka mataifa zaidi ya 70 duniani, Mkutano huu umeanza Septemba 05, na unatarajiwa kutamatika Sepmtemba 08, 2023.

By Jamhuri