Na Mwandishi Wetu,Jamhurimedia,Dar

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amewahamasisha viongozi wa Chama hicho kwa ngazi mbalimbali kujenga utamaduni wa kuwatembelea na kuwatambua viongozi wa Shina, Tawi na Kata pamoja na kushiriki vikao vya Chama kwenye ngazi hizo.

Kinana ameyasema hayo leo alipokwenda kujitambulisha kwa viongozi wa CCM Tawi la Masaki pamoja na viongozi wa Kata ya Msasani jijini Dar es Salaam waliochaguliwa hivi karibuni kupitia Uchaguzi wa ndani ya Chama unaondelea.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana akizungumza k katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Msasani pamoja na viongozi wa Chama Tawi la Masaki, jijini Dar es Salaam alipokwenda kujitambulisha na kuwatambua viongozi wake katika ngazi hiyo. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM)

“Nimekuja kuwapongeza, kuwatambua na kujitambulisha kwa viongozi mliochaguliwa katika uchaguzi huu unaondelea ndani ya Chama chetu. Na nawahimiza viongozi wote kwenda kwenye matawi yao, mabalozi wao, kwenye kata zao ili wajulikane na washirikiane na matawi yao na viongozi wa matawi na kata. Tunataka viongozi watambue viongozi wanaowaongoza,” amesema Kinana.

Mwanachama wa kata ya Msasani akizungumza 

Ameafanua yeye ni mwanachama wa Tawi na Kata hiyo, hivyo anawajibu wa kuwajua viongozi wake kwa sababu kila kiongozi anaye kiongozi mwingine anayemuongoza.

“Nimekuja kutambua viongozi wangu, kwa sababu kila kiongozi ana kiongozi wake anayemuongoza. Makamu Mwenyekiti ana viongozi wake. Unajua kuna watu wanaweza kufikiri Makamu Mwenyekiti hana kiongozi au Mwenyekiti wetu Taifa hana kiongozi, Mwenyekiti wa Taifa ana tawi lake, ana balozi wake.

“Leo hii nimeamua kujitambulisha na kuwatambua viongozi wa tawi na kata, siku nyingine rasmi nitapanga kwenda kuonana na wanachama wenzangu na kwenda kutambua balozi wangu,” alisema Kinana alipokuwa akijitambulisha, mimi ni mwanachama wa Kata hii nina wajibu wa kuwajua viongozi wangu.

Mwenyekiti wa Tawi la masaki 
Ndugu, Rafael Kamana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Tawi la Masaki jijini Dar es Salaam waliochaguliwa hivi karibuni kupitia Uchaguzi wa ndani ya Chama unaondelea.akizungumza