Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) , umemchagua kwa kishindo askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Drk Alex Malasusa kuwa mkuu mteule mpya wa KKKT kupokea nafasi ya Askofu Dk Frederick Shoo aliyestaafu baada ya kumaliza muda wake wa uongozi.

Mwenyekiti wa uchaguzi huo iliyofanyika Arusha Askofu Amon Mwenda amesema askofu Malasusa ameshinda kwa kura 167 sawa na asilimia 69.3 ya kura zote 241 zilizopigwa huku askofu Abednego Kesho Mshahara akipata kura 73 sawa na asilimia 30.3.

Askofu Malasusa anarejea kwenye nafasi hiyo tena ,nafasi ambayo alikwisha tumikia kwa uwongozi kati ya mwaka 2007 hadi 2015 alipomaliza muda wake na kumkabidhi Dkt Shoo.

By Jamhuri