Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) iliyopo Mkoani Geita watatoa  huduma za tiba mkoba zijulikanazo  kwa  jina la  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya kliniki maalumu za uchunguzi, matibabu ya magonjwa ya Moyo na upasuaji wa mishipa ya damu  kwa wananchi wa mkoa wa Geita na mikoa ya jirani.

Kliniki hizo zitafanyika kwa watu wazima tarehe 19-23/02/2024 kuanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato.

Tunawaomba wagonjwa wenye matatizo ya moyo, mishipa ya damu ya miguu na mikono wafike katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu.

Aidha Taasisi inawasisitiza wananchi watumie nafasi hii adhimu kwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ili wajue kama wana matatizo ya moyo au mishipa ya damu ya mikono na miguu  ili waanze matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0768492622, 0767665548 na 0718023931.  

 “Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.