Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Gerald Kusaya ametangaza watuhumiwa tisa wakiongozwa na Mmiliki wa Kambiaso Sports Academy, Alhaj Kambi Zubeir Seif pamoja na Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Mwalami Sultan kuhusika kukamatwa na dawa za kulevya aina ya Heroin yenye jumla ya Kilo 34.89.

Kusaya ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 15,2022.