Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

Upungufu wa maji na kukatikakatika kwa Nishati ya Umeme ,imekuwa gumzo na kilio kwa Madiwani wa Kibaha Mjini katika baraza la madiwani ,na kudai ni kero ya muda mrefu iliyo na ukakasi kwenye ufumbuzi wake.

Agustino Mdachi diwani wa Kata ya Pangani na Mohamedi Chamba diwani wa kata ya Viziwaziwa walisema kero ya Maji na Nishati ya Umeme imekuwa kero kubwa kwa wananchi hali inayoathiri utendaji kazi ,;muda mrefu wanatumia kutafuta Maji sanjali na kukatika Umeme kukiathiri uzalishaji mali kwa wajasiliamali.

Hoja hiyo imekuwa msumali wa moto baada ya kuungwa mkono na Madiwani wote na kuziaguza taasisi husika kushughulikia huduma hizo .

Awali akiwasilisha hoja ya ziara ya Madiwani wa Viti maalum,Katibu wa Kamati hiyo Shufaa Mshana alisema ziara yao imebaini vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia,Kero za miundombinu ya Barabara na Mikopo ya asilimia 10 ikishindwa kurudishwa kwa wakati na vikundi nufaika ambapo takribani kiasi cha Shilingi Bilioni moja kipo mikononi mwa wakopaji.

Vilevile madiwani wamekuwa wachungu kwa wakala wa Barabara nchini TANROAD kutokana na ucheleweshaji wa fidia kwa wananchi wanapofanya utekelezaji wa ujenzi wa Barabara.

Kitengo cha kujenga Barabara kwa muda mrefu ilielezwa kuwa hakiwafurahishi Madiwani hao kutokana na kuwa kero kwa wananchi wanapotekelezaji shughuli zao za Wananchi.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha ,Selina Wilson alisema wananchi wameoneshwa kutofurahishwa na kitendo hicho kwani wanahitaji Maendeleo.

Nae Diwani wa Kata ya Visiga Kambi Legeza alishauri matengenezo ya Barabara ya zamani ya Morogoro ipewe kipaumbele cha matengenezo kwani imekuwa mbadala kwa Barabara ya Sasa inapokuwa na foleni.

By Jamhuri