Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Pwani

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ameziagiza wilaya, Halmashauri kujiwekea mipango kazi, mikakati ambayo inakwenda kuboresha mazingira ya kibiashara ili kuinua sekta ya biashara katika kuongeza pato la Taifa .

Aidha ametoa rai kuimarisha fursa za kiuchumi ili kuleta matokeo chanya.

Akifungua mkutano wa Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani, lililofanyika ukumbi wa mikutano Jengo la Wauguzi ,Kibaha Mjini Mkoani humo, Kunenge ameeleza mkoa unapaswa kuwa tofauti ,kwa kujipambanua kutekeleza mikakati wanayojiwekea ili kuleta tija.

“Tunaona Rais wetu, Dkt.Samia Suluhu Hassan anavyofanya kazi kubwa kuweka Mazingira bora ya kibiashara nchini , na kusikiliza vilio vya wafanyabiashara kutatua baadhi ya kero zao, Rais amekuwa wa moto na hapoi “

“Yatupasa tuendelee kushirikiana nae kuboresha na kuimarisha fursa za kibiashara na uchumi “amsema Kunenge.

Mkuu huyo wa mkoa, amesema mkoani unaendelea kuboresha miundombinu ya barabara,maji, Nishati ya umeme,kutenga ardhi ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji,yote ikiwa kuweka Mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

Vilevile aliomba mifumo ya Taasisi za Serikali zinazokusanya mapato ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweka Mazingira rafiki ya ukusanyaji mapato ili kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara.

Awali Mwenyekiti wa TCCIA Mkoani Pwani,Said Mfinanga aliiomba TRA mkoa kujenga Mazingira rafiki ya ukusanyaji kodi pasipo kudai madeni kwa kutumia nguvu.

“Wafanyabiashara ni miongoni mwa wachangiaji pato la Taifa,sisi sio wezi,tunaomba ukusanyaji wa kawaida kwa njia za kirafiki”amefafanua Mfinanga.

Mfinanga pia alitaka TRA kila wilaya kuandaa Semina ili kuelimisha wafanyabiashara kujua namna ya kujikwamua na changamoto wanazozisababisha kwa TRA na Kuwa na uelewa wa mabadiliko ya sheria ya ulipaji wa kodi mpya.

Meneja wa TRA Mkoani Pwani,Masawa Masatu alieleza,Wana Utaratibu wa kudai madeni kisheria na kwa Utaratibu bila usumbufu.

Alielezea,wanajipanga kutembelea mkoa mzima kutoa elimu ya mabadiliko ya kisheria ya ukusanyaji kodi na wanashughulikia madeni yote ya nyuma ambapo wanasubiria Mamlaka na Utaratibu maalum kushughulikia jambo hilo.

Dkt. Riziki Nyello ,Mkurugenzi wa Mazingira ya Biashara wa TNBC alielezea , katika kuboresha Mazingira ya kibiashara tozo 232 kati ya 580 zilizoainishwa katika biashara zimefutwa.

Pamoja na hilo, ameeleza Mkoa wa Pwani ni mkoa wa kimkakati, na ameupongeza kuboresha Mazingira ya kibiashara kuinua uchumi.

Nyello alihimiza, kuimarisha tathmini ya majadiliano ya mabaraza ya kibiashara na kuondoa vikwazo katika kuboresha Mazingira ya kibiashara pasipo Kuwa vikwazo

By Jamhuri