Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

MAKUMI elfu ya akina mama na familia zao wa mikoa mitano ya Dodoma, Morogoro, Mwanza, Arusha na Geita, watanufaika na kampeni iliyozinduliwa jijini Dodoma na kampuni ya Lake Energies Group iliyopewa jina la ‘Tumtue Mama Kuni Kichwani’ kwa kuwagawia mitungi 13,500 ya gesi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dodoma leo Septemba 1, 2023, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group, Matina Nkurlu, alisema kuwa uamuzi wao huo umelenga kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa.

Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (wapili kushoto)Mbunge wa Bahi,Kenneth Nollo na Mbunge wa Mpwapwa,George Malima wakibadilishana mawazo na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group,Matina Nkurlu (wapili kulia) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ”Kumtua Mama kuni kichwani” iliyozinduliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa nishati vijijini (REA) yenye lengo la kusambaza mitungi ya gesi 13,500 kwa mikoa ya Dododma,Mwanza,Geita,Morogoro na Arusha, Ikiwa na lengo la utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa nchini.

“Lake Energies tumeona ni vema kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), katika kampeni ya utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa na tayari tumeshasambaza mitungi katika mikoa ya Arusha, Morogoro, Mwanza na Geita.

“Pia, kampeni hii inalenga kumwondolea mwanamke wa kitanzania adha ya kutumia muda mwingi kwenda kutafuta kuni au mkaa wa kupikia na hivyo kuepukana na hatari za huko maporini na badala yake kupata muda mwingi wa kutunza familia na ndoa zao,” amesema Nkurlu.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake ambao majimbo yao yamehusishwa katika kampeni hiyo, Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Job Ndugai, aliishukuru Lake Energies kwa mpango wao huo, akiyataka na makampuni mengine kuiga mfano huo wa kumuunga mkono Rais Samia.

Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (wapili kulia)Mbunge wa Bahi,Kenneth Nollo na Mbunge wa Mpwapwa,George Malima wakikabidhiwa mtungi wa gesi na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group,Matina Nkurlu(kulia)ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa kampeni ya”Kumtua Mama kuni kichwani”iliyozinduliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa nishati vijijini(REA) yenye lengo la kusambaza mitungi ya gesi 13,500 kwa mikoa ya Dododma,Mwanza,Geita,Morogoro na Arusha, Ikiwa na lengo la utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa nchini.

“Kwa niaba ya wabunge wenzangu wa Mkoa wa Dodoma, tunawashukuru sana Lake Energies kwa uamuzi wenu huu wa kuamua kugawa mitungi ya gesi kwa akina mama wa mkoa wetu kwa kushirikiana na serikali yetu.

“Kama ilivyo kwa mikoa mingine, akina mama wa Dodoma wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenda kutafuta kuni za kupikia hali inayowachosha, lakini pia ikichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira. Tunawashukuru sana,” alisema Ndugai ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Musukuma, alisema kuwa msaada huo umekuja wakati mwafaka ambao Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeonekana kuwajali mno wanawake wa Tanzania kwa kuwapunguzia kama si kutokomeza baadhi ya kero zinazowakabili, ikiwamo ya kutumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa wa kupikia.

“Kwa niaba ya wanawake wa Jimbo langu la Geita, tunawashukuru sana kwa kutufikiria katika kampeni yenu hii, Mungu awabariki sana,” amesema Musukuma.

Naye mwakilishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Injinia Michael Kyessi, ameitaka jamii ya Watanzania kubadilika kwa kugeukia katika matumizi ya gesi kwa kupikia na shughuli nyinginezo zinazohitaji nishati ya moto badala ya kuni na mkaa.

“Ukataji miti umekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira nchini, hivyo tunawashauri wanawake na watanzania kwa ujumla, kugeukia katika matumizi ya gesi badala ya kuni na mkaa kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali yetu ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kampeni ya ‘Kumtua Mama Kuni Kichwani’.

“Wanufaika wa mitungi hii 13,500 katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Morogoro, Geita na Mwanza, wakawe mabalozi wa wenzao katika maeneo yao kuhakikisha jamii inaachana kabisa na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa,” amesema.

Mbali ya bidhaa ya gesi, Lake Energy Group wanajishughulisha pia na uuzaji na usambazaji wa petrol, dezeli, mafuta vilainishi ya mashine, nondo na bidha nyinginezo pamoja na kutoa huduma ua usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (wapili kulia)Mbunge wa Bahi,Kenneth Nollo na Mbunge wa Mpwapwa,George Malima wakikabidhiwa mtungi wa gesi na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group,Matina Nkurlu(kulia)ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa kampeni ya”Kumtua Mama kuni kichwani”iliyozinduliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa nishati vijijini(REA) yenye lengo la kusambaza mitungi ya gesi 13,500 kwa mikoa ya Dododma,Mwanza,Geita,Morogoro na Arusha, Ikiwa na lengo la utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa nchini.
Kutoka shoto Mbunge wa Bahi,Kenneth Nollo, Mbunge wa Mpwapwa,George Malima, Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai pamoja na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group,Matina Nkurlu wakionesha mitungi ya gesi mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya”Kumtua Mama kuni kichwani”iliyozinduliwa na kampuni ya Lake Energies kwa kushirikiana na wakala wa nishati vijijini(REA) yenye lengo la kusambaza mitungi ya gesi 13,500 kwa mikoa ya Dododma,Mwanza,Geita,Morogoro na Arusha, Ikiwa na lengo la utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa nchini.