*Watembea kilomita tano kutafuta maji

Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia,Lindi

Wanakijiji cha wa Mpotora Wilaya ya Kilwa, Kata ya Pande Plot ,wameiomba serikali kuwapatia maji safi na salama.

Akizungumza na JAMHURI kwa niaba ya wenzake Selemani Hamza amesema kijiji chao, kimekuwa na shida ya maji kiasi cha kuwafanya wawe hatarini kupata magonjwa ya milipuko na kugongwa na nyoka wakati wanapokwenda kutafuta maji.

Hamza amesema tatizo la maji katika kijiji chao,limekuwa sugu na watu wamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilometa tano kufuata maji kwenye kata .

Amesema changamoto ya maji imewafanya baadhi wanawake kushinda visimani ,wakati mwingine hata kuhatarisha usalama wao kutokana na changamoto.

“Watu wamekuwa wakikoga kwa hatua kwa sababu maji yanayopatikana yanakuwa machache na kwa matumizi ya familia lazima wajibane matumizi”amesema Hamza

Amedai kwa upande wa watoto wa shule wamekuwa na wakati mgumu ,kwasababu wakati mwingi wamekuwa wakiambatana na mama zao kwenda kutafuta maji.

Amesema kadhia hiyo imesababisha baadhi ya watoto, kurudi usiku na wengine kuhatarisha maisha yao kwa kugongwa na nyoka nyakati za kurudi .

Changamoto ya maji inasababisha migogoro mingi kwenye familia, hata wakati mwingine inasababisha kutengana
Muhandisi wa maji wilaya ya Lindi Ramadhani Mabura amesema. katika kata hiyo ya pande tayari wana mradi wa maji bado
“utaendelea kwenye vijiji wanakwenda kwa awamu na wanafika katika vijiji vyote mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya mwaka huu”amesema .