Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Kimataifa wakati wa Wimbo wa Umoja wa Afrika (AU) na ule wa Taifa wa Kenya ukiimbwa mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Nairobi nchini Kenya tarehe 05 Septemba, 2023 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23).
Viongozi kutoka Mataifa mbalimbali Duniani wakiwa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23) tarehe 05 Septemba, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23) Nairobi nchini Kenya tarehe 05 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23) Nairobi nchini Kenya tarehe 05 Septemba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23) Nairobi nchini Kenya tarehe 05 Septemba, 2023

By Jamhuri