Mahasimu wa kubwa kutoka jiji la London, Totenhum Spurs na Arsenal leo wanakuta kwenye mchezo wa Ligi kuu Uingereza, Totenhum watakuwa nyumbani ikiwakaribisha Arsenal majira ya saa 9: 30 mchana.

Mchezo huo unaonekana kuwa mgumu kwa timu zote mbili licha ya Totenhum kupewa nafasi kubwa ya Kuibuka na ushindi katika Mchezo huo kutokana na Spurs msimu huu kuwa fit katika idara zote ndani ya Uwanja.

Spurs ipo nafasi ya 5 ikiwa na point 49 nyuma ya Chelsea ikiwa na point 50, endapo Spurs itaibuka na ushindi basi itapaa mpaka nafasi ya 3 na itafikisha point 52.

Arsenal ipo kwenye nafasi ya 6 ikiwa na point 45, hata ikishinda mechi ya leo bado itabaki hapo hapo kwenye nafasi ya sita kwani itafikisha point 48 ambazo hazitaifanya kupanda nafasi yoyote kwenye msimamo wa Ligi kuu Uingereza.

Katika michezo iliyopita Arsenal Waliwatandika Evertoon 5-1, huku Spurs ilitoka Sare na Liverpool kwa Kufungana magoli 2-2

 

RECORD ZA MECHI ZA TOTENHUM SPURS VS ARSENAL

08 Nov 2015 Arsenal v Tottenham Hotspur 1-1 Premier League
05 Mar 2016 Tottenham Hotspur v Arsenal 2-2 Premier League
06 Nov 2016 Arsenal v Tottenham Hotspur 1-1 Premier League
30 Apr 2017 Tottenham Hotspur v Arsenal 2-0 Premier League
18 Nov 2017 Arsenal v Tottenham Hotspur 2-0 Premier League

MSIMAMO WA LIGI KUU UINGEREZA

 

Please follow and like us:
Pin Share