LIVERPOOL YAZIDI KUFANYA MAAJABU EPL, YAITWANGA LEICESTER 2-1

Kikosi cha Liverpool kimeendelea kuonesha dhamira ya kukirejesha kikombe cha Ligi Kuu England kwa kuicharaza Leicester City mabao 2-1 ikiwa kwao.

Mabao ya Liverpool yamepachikwa kimiani na Sadio Mane mnamo dakika ya 10 pamoja na Robert Firmino katika dakika ya 45.

Bao pekee la Leicester limewekwa nyavuni na Rachid Gezzal kwenye dakika ya 63 na likiwa la kwanza kwa kipia Mbrazil, Allison Becker kufungwa tangu awasili kwenye ligi hiyo na Liverpool.

Baada ya ushindi huo, Liverpool sasa imezidi kujiweka kileleni kwa kufikisha alama 12 ikiwa nafasi ya kwanza huku Tottenham na Chelsea zikifuatia.

1917 Total Views 4 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!
Show Buttons
Hide Buttons