Maandalizi ya utoaji tuzo za wanamichezo bora waliofanya vizuri mwaka 2025 zinazotolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) yamefikia 90% ambapo shughuli hiyo itafanyika katika ukumbi wa The Super Dome Masaki, tarehe 9 Mei, 2026 kuanzia saa 12 jioni.

Akizumgumza kuhusu tuzo hizo, Katibu Mtendaji wa BMT Bi. Neema Msitha ameeleza kuwa, Kamati ya maandalizi ya utoaji wa tuzo hizo imejiandaa kikamilifu kufanikisha shughuli hiyo ya kuwaenzi na kuwasherehekea wanamichezo hao waliofanya vizuri kitaifa na kimataifa.

Bi. Msitha amesema mwaka huu kuna tuzo mbalimbali 21 ukinganisha na mwaka 2024 ambapo zilikuwa 20 na kuongezeka tuzo moja ya Mwanahabari Nguli wa Michezo.

Amewahimiza Watanzania kuendelea kupiga kura kuhusu Tuzo ya Mchezaji Bora Chaguo la Watu kupitia WhatssApp (+255-689-525363)