Na Helena Magabe Jamhuri media Tarime

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali za mitaa (LAAC), Stanslaus Mabula ameagiza Halmashauri kusimamia mradi wa soko na itakapofika Mei 17,2024 ujenzi uwe umeisha.

Ameiomba Halmashauri hiyo kuipatia kampuni ya Mohamadi Builders pesa ili wakamilishe ujenzi kwa wakati na wasimamie kuhakikisha soko linaisha na linaanza kutumika.

Mkandarasi mshauri Leonard Mwangoka akionyesha ramani ya soko.

Amesema katika akiba ya shilingi milioni 200 waliyonayo hazina wanaweza kumpa ili ifikapo Mei 17, 2024 soko hilo liwe limekamilika kwani kuchelewa kwa kazi kunasababisha ongezeko la gharama hivyo mradi huo unatakiwa kukamilika kwa muda uliopangwa .

Mkandarasi mshauri wa mradi huo injinia Leonard Mwangoka amemweleza Mabula kuwa mradi umefikia asilimia 7 ya ujenzi ambapo wanatarajia kukamilisha ujenzi wa mradi huo ifikapo Mei 17,2024 na kuanza kutumika.

Lakini Mabula amesema si rahisi mradi huo kukamilika ndani ya miezi miwili kufuatia ukubwa wa kazi iliyobaki na uchache wa wafanyakazi hivyo amemshauri Mkandasi mwenye Mradi huo, John James kuongeza wafanyakazi wa kutosha ili ujenzi ufanyike kwa haraka.

Amesisitiza kuwa mkataba hautaongezwa tena kwani umeongezwa mara nne na kuwachelewesha wafanyabiashara kutumia soko kwa mwaka mzima licha ya kuwa wamekuwa wavumilivu lakini hata wakiambiwa maneno matamu kiasi gani hayawasaidia wanachotaka ni soko.

” Kama shida ni changamoto za kifedha wamwandikieni Rasi satificate (cheti) na kufuatilia kwa kupiga simu kwani satificate haitakiwi kukaa wiki tatu usipofuatilia mara nyingi huwa zinawekwa pembeni na unaambiwa walisahau” amesema.

Hata hivyo ameiomba TAMISEMI isitoe miaka 10 ya ukamishaji wa miradi bali itoe hata miaka 40 kwa miradi hiyo ni ya Serikali kwa kutoa miaka michache wakurugenzi wanapata presha (pressure) ya kukimbizana na muda wa kukamilisha mradi hali inayopelekea wakati mwingine miradi kutokuwa bora.

Mjumbe wa Kamati hiyo Daimu Iddi Mpakate ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduma kusini mkoani Ruvuma amewashauri wakandarasi wa mradi wa soko kuongeza nondo nene kwenye vibanda vya juu na kuweka silingboard kwa ajili ya tahadhari ya usalama.

Amewashauri kuongeza wafanyazi kazi iende haraka vinginevyo kufikia Mei 17 mradi utakuwa bado haujakamilika kwani kazi bado ni kubwa na wafanyakazi ni wachache hivyo waongeze wafanyakazi.

By Jamhuri