Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanikiwa kutoa kipande cha plastiki kwenye pafu la kushoto la mtoto mwenye umri wa miaka 11, kupitia kifaa maalumu kinachoitwa Flexible Bronchoscopy.

Kifaa hicho kinatumia mpira laini wenye kamera ya uchunguzi wa mapafu bila kuhitaji mgojwa kupewa dawa za using ili.

Akizungumza kwa niaba ya timu ya watalaam Daktari Bingwa wa Mapafu Dkt. Mwanaada Kilima amesema kuwa mtoto huyo alikuja na dalili za kikohozi cha muda mrefu na siku zote amekuwa akiambiwa ana homa ya mapafu mpaka alipokuja Muhimbili na kupatiwa matibabu sasa kikohozi kimeacha na hali yake inaendelea vizuri na tunatarajia kumruhusu ili aende nyumbani kuendelea na maisha.

Kwa upande wa nama mzazi wa mtoto Edward Bi. Florence Joseph amesema kuwa wamekuwa wakihangaika Hospitali mbalimbali kwa mwaka mmoja na miezi kumi na moja bila kupata matibabu mpaka walipopewa rufaa kuja Muhimbili,

Florence ameshukuru kwa huduma nzuri
na upendo wa hali ya juu aliopata kutoka kwa watoa huduma.

Please follow and like us:
Pin Share