Na Albano Midelo, JamhuriMedia, Ruvuma 

Pato la Taifa katika Mkoa wa Ruvuma limeongezeka  kutoka shilingi bilioni 2.37 mwaka 2012 hadi kufikia bilioni 6.39 mwaka 2022.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uchumi wa Kanda ya kusini Mashariki ukiwemo Mkoa wa Ruvuma unaendelea kuimarika.

Kulingana na NBS  Pato la Taifa (GDP) katika kanda hiyo limekuwa linaongezeka mwaka hadi mwaka na kufanya kanda hiyo kuchangia wastani wa asilimia 10.5 ya Pato la Taifa katika Mkoa wa Ruvuma.

Kwa mujibu wa NBS ongezeko hilo limechangiwa zaidi na uzalishaji katika shughuli za kilimo na madini.

Katika mwaka 2022,Mkoa wa Ruvuma ulichangia asilimia  3.8 ya Pato la Taifa na kuwa juu ya mikoa mingine ya Kanda ya Kusini Mashariki iliyochangia kati ya asilimia 2.0  na asilimia 2.8 .

Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita wastani wa pato kwa mtu GDP  katika wa Ruvuma limeongezeka  kwa Zaidi ya maradufu na kuwa juu ya wastani wa pato kwa mtu kitaifa.

Hata hivyo kulingana na NBS wastani wa pato kwa mtu kwa mwaka kwa Mkoa wa Ruvuma uliongezeka kutoka shilingi 1,725,241 mwaka 2012 hadi kufikia shilingi 3,458,329 mwaka 2022.

Mkoa wa Ruvuma ni wa tisa katika kuchangia kwenye pato la Taifa kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara.

By Jamhuri