Na Helena Magabe, JamhuriMedia,Tarime

MADIWANI katika Halmashauri ya Wilaya Tarime wamejipongeza kuvuka lengo ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao cha baraza la Madiwani walisema wanatakiwa kujipongeza kwa kuvuka lengo kwa asilimia 116.

Makisio ya ukusanyaji mapato yalitakiwa kuwa milioni 896.lakini wamefanikiwa kukusanya bilioni 4 hali iliyofanya Madiwani kujipogongeza kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji mapato.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Simon Keresi amewataka Watumishi kufanya kazi kwa kusimamia vizuri miradi kwani fedha nyingi ziko kwenye miradi.

Amesema watalamu wafatilie kila. Kata na kila Kijiji fedha za miradi zinapokuja zisibaki bila kufanya kazi na kurrudi bila miradi kukamilika.

Amemtaka Mkurugenzi kuwambia watalamu wake wafatilie kwa karibu miradi ambayo haijakamirika ikamilike na kufanya kazi haraka.

Aidha amesema kuna madawati yanayotokana na fedha za CSR yalitakiwa kukabidhiwa leo lakini yatakabidhiwa katika kikao cha robo ya tatu kijacho pamoja Gari ambalo poa nilitokana na fedha za CSR.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Solomon Shati amesema bila Madiwani kushiikiana na watumizi kusingekuwa na hati safi.

Amesema Watalamu wafatilie kwa haraka miradi ambayo haijakamilika na kuhakikisha inamalizika kwa wakati na kutumika.

By Jamhuri