Na Padri Dk. Faustine Kamugisha

Moyo ni sababu ya mafanikio. Unapoweka
moyo wako wote katika lile unalolifanya
utafanikiwa. “Fanya kazi kwa moyo wako
wote, na utafanikiwa – kuna ushindani
mdogo,

” alisema Elbert Hubbard.

Kuna methali ya Tanzania isemayo: “Moyo
uutulize sehemu moja kama mbwa
anapopikiwa panya.” Kinachobainishwa
hapa ni kuwa na moyo usiogawanyika.
Mtaka yote kwa pupa hukosa yote.
“Tia moyo wako, akili na roho yako hata
katika matendo madogo sana. Hii ni siri ya
mafanikio,

” alisema Swami Sivananda.
Hakikisha kuna utulivu moyoni. Mtu aitwaye
Ikengya aliulizwa: “Ikengya mbona
umenyamaza?” Alijibu: “Kelele imezidi
moyoni.” Ikengya hakuwa na utulivu

moyoni.
Kuna methali ya Wahaya isemayo: “Moyo
ulipolala ndipo miguu huamkia.” Weka moyo
wako kwenye shughuli itakayokuinua,
utaamkia huko. “Kila mmoja ameumbwa
kwa ajili ya kazi maalumu na shauku ya
kufanya kazi hiyo imetiwa kwenye kila
moyo,

” alisema Rumi. Kuwa na shauku ya
kufanya lile litakalokuinua. “Kila
unapokwenda, nenda na moyo wako wote,

alisema Conficius.
“Ni moyo unaomfanya mtu awe tajiri. Ni tajiri
kadiri alivyo, na si kadiri ya alichonacho,

alisema Henry Ward Beecher.
Kinachobainishwa hapa ni: kuwa ni zaidi ya
kuwa na. Kuwa mwema, kuwa mwenye utu
ni zaidi ya kuwa na kitu.
Moyo ni sehemu ambapo upendo unaishi.
Moyo ni maskani ya utu, upendo, msamaha
na huruma. “Moyo mwema una thamani ya
dhahabu,

” alisema mshairi na mwanafalsafa

Shakespeare.
“Moyo wenye shukrani ni mwanzo wa
ukubwa. Ni kielelezo cha unyenyekevu. Ni
msingi wa kuendeleza fadhila kama sala,

imani, ujasiri, kuridhika, furaha, upendo na
ustawi,

” alisema James E. Faust. Yote
yakishasemwa jua kuwa moyo ni kiini cha
hisia. Moyo ni undani wa tabia ya mtu.
“Kichwa kizuri na moyo mzuri ni
mchanganyiko wenye nguvu,

” alisema
Nelson Mandela. Unapokutana na watu
wanapima kichwa chako. Mnapoachana
wanapima moyo wako. “Kuna hekima ya
kichwa na hekima ya moyo,

” alisema

Charles Dickens.
Kupenda wateja ni hekima ya moyo. “Kila
mtu anaweza kupenda ua la waridi, lakini
yahitaji moyo mkubwa kupenda jani,

alisema Askofu Mkuu Fulton Sheen wa
Marekani. Kuna methali ya Wahaya
isemayo: “Muuza chumvi anuke lakini
chumvi iwe tamu.” Ni kejeli kwa mtu
anayependa chumvi zaidi ya muuza chumvi.
Wape watu moyo uliojaa furaha. Moyo wako
uwe sumaku ya kuvuta wateja na marafiki
wa kweli. “Kuna sumaku katika moyo wako
ambayo itawavuta marafiki wa kweli.
Sumaku hiyo ni kutokuwa mbinafsi,
kuwafikiria wengine kwanza; unapojifunza

kuishi kwa ajili ya wengine, wataishi kwa ajili
yako,

” alisema Paramahansa Yogananda.
Unaweza kuwavuta watu kwa tabasamu.
Tabasamu haina gharama yoyote. Matokeo
yake yana gharama. “Tabasamu ni ufunguo
ambao unaingia kwenye kufuli ya moyo wa
kila mtu,

” alisema Anthony J. D’Angelo.

Kuna tabasamu ambayo huwa siitoi hovyo
hovyo. Niliwatembelea wagonjwa
hospitalini, mmoja nikampa tabasamu hiyo.
Wakati natoka, nilikohoa. Mgonjwa
alitamka: “Nipo, unaniita.” Ni tabasamu
iliyokuwa na matokeo chanya.
Moyo wako uwe moyo wenye ndoto na
maono, bila shaka utafanikiwa. “Moyo bila
ndoto ni kama ndege bila manyoya,

alisema Suzy Kassem. Ili kufanikiwa
unahitaji maono na maono ni suala la moyo.
“Nafikiri zawadi kubwa sana ambayo Mungu
aliwahi kumpa binadamu si zawadi ya
kuona bali zawadi ya maono. Kuona ni kazi
ya macho, lakini maono ni kazi ya moyo,

alisema Mchungaji Myles Munroe.
Moyo ni maskani ya maono. “Kataa kuwa
mtu wa wastani. Wacha moyo wako upae

kwa juu kadiri uwezavyo,

” alisema Aiden

Wilson Tozer.

Mwisho

By Jamhuri