Na Francisco Peter, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Imeelezwa kuwa Chuo cha Bandari kinafasi pana katika masuala mapana sekta ya uchukuzi bandari nchini.
Mazungumzo na mijadala kuhusu maandalizi ya sekta ya usafirishaji na bandari kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 yameendelea kuangazia umuhimu wa elimu inayozalisha ujuzi, weledi na uwajibikaji kwa wanafunzi, wahitimu na watendaji wa sekta hiyo.
Katika maelezo yaliyotolewa kitaaluma jana jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji Umoja wa Mwawakala wa Meli Tanzania Abel Uronu, mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika tasnia na ufundishaji alisisitiza kuwa .
Uronu ambaye alikuwa ndiye Mgeni Rasmi katika akizunguza mbele ya wahitimu waliosoma katika Chuo hicho amesema wanafunzi na vyuo wanapaswa kubadilika ili kuendana na mahitaji halisi ya soko la ajira na maendeleo ya nchi ifikapo mwaka 2050.
“Wahitimu wengi kuwa na vyeti vizuri iliwasikumbane na changamoto wanapofanyiwa usaili au kuingia kwenye mazingira ya kazi kwa kushindwa kujieleza ipasavyo wanaitaji wajitaidi kuwa na misingi imara ya kiutendaji, kama vile uelewa wa nyaraka za msingi za uondoshaji mizigo bandarini,”amesema Uronu.
Aidha, aligusia ujio na matumizi ya Akili Unde (AI), akibainisha kuwa ingawa teknolojia hiyo inaweza kutoa majibu ya haraka kwa wanafunzi, utegemezi mkubwa usio na fikra za kina na uelewa binafsi unaweza kumfanya mwanafunzi ajidanganye kuwa anajua kumbe hana uwezo wa kutekeleza majukumu anapokuwa kazini.
Katika mjadala huo, ilielezwa pia kuwa mifumo ya upimaji katika baadhi ya mamlaka za elimu imekuwa ikiipa uzito mkubwa zaidi kwenye coursework ikilinganishwa na mtihani wa mwisho, hali inayotaka uadilifu na bidii ya kujifunza ili ujuzi unaopatikana uwe wa kweli na wenye tija.
Kwa upande wa sekta ya bandari na usafirishaji,RobertMallami Mwenyekiti wa Alluminas alifafanua kuwa kuwa kufikia malengo ya Dira ya 2050.
Ikiwemo mchango mkubwa wa sekta binafsi na ukuaji wa uchumi kunategemea siyo tu miundombinu na mitambo, bali pia nguvu kazi yenye mafunzo bora, weledi, uzingatiaji wa sheria na taratibu, pamoja na uwezo wa kupunguza ucheleweshaji na hasara zisizo za lazima katika mnyororo mzima wa usafirishaji na ugavi.
Viongozi na wadau walioshiriki waliwapongeza waandaaji na wazungumzaji kwa kuwaleta pamoja wahitimu na wanafunzi wa sasa ili kujadili namna ya kujiandaa vyema kuelekea 2050, huku wakisisitiza kuwa elimu ya vitendo na ujuzi stahiki ndiyo nguzo kuu ya mafanikio ya mtu binafsi na taifa.



