Na Magrethy Katengu,Jamhuri Media, Dar es Salaam

Chama cha ACT Wazalendo kimemwomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kujionea hali halisi Rufiji na Kibiti waliokumbwa na janga la mafuriko huku malighafi zao zikiharibika ikiwemo makazi na mashamba yao.

Ombi hilo amelito leo Aprili 7,2024 jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu kivuli wa chama hiko Mhe Isihaka Machinjita ambapo amesema siku kadhaa alifanya ziara Rufiji na Kibiti maeneo ya makazi ya watu ambao wamezungukwa na Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere na kujionea maeneo yaliyozunguka Bonde la mto Rufiji yakiwa yamezungukwa na maji yote hakuna kinachoonekana .

Machinjita amebainisha kuwa walipofanya mahojino walibaini kuwa Bwawa la Umeme la mwalimu nyerere baada ya maji yote kuelekezwa katika Bwawa hilo maji yamejaa kupitiliza kiwango kinachotakiwa hivyo ikabidi baadhi ya milango ya Bwawa ifunguliwe kuruhusu maji yatoke yasije yakaleta madhara hivyo yakaelekezwa katika katika Bonde la mto Rufiji lakini yakawa mengi na mengine kufika kwenye makazi ya watu na kusababisha mafuriko

Sambamba na hali hiyo watu wamekimbilia kuishi mashuleni hivyo Serikali inatakiwa kuliangalia suala hilo kwa makini kwa kuwalipa fidia wananchi wake ili waweze kumudu gharama za maisha kwani mali zao zimeteketea na maji huku mvua nazo zinaendelea kunyesha.

” Ukanda wa Kibiti na Rufiji eneo linalozunguka Bonde la Mto Rufiji hasa lililopo karibu na Bwawa la.kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere kuna hali mbaya sana zaidi ya kata 12 zimeathirika vibaya na maji mazao, makazi ,huduma za msingi za kijamii vimeharibiwa vibaya wananchi wengi wamejihifadhi kwenye shule ambazo hazijapatwa na maji hali ni mbaya sana”amesema Waziri Mkuu Kivuli.

Hata hivyo ACT wazalendo wameishauri serikali kutenga bajeti (fedha) ya kutosha ili kujenga uwezo.idara ya maafa na kuongeza ufanisi wa usimamizi pia ni muhimu kujengea uwezo kwa kutumia teknolijia juu ya kufuatilia maafa sehemu mbalimbi za nchi

Aidha kumekuwa na majanga ya maafa yakijirudia mara kwa mara ikiwemo kuungua masoko mafuriko hivyo serikali haina budi kuchukua hatua za tahadhari kukinga majanga yanayoweza kujitokeza huku kukiwa na mipango ya kabla kukabiliana badala ya kusubiri majanga yatokee ndiyo wasogee kutoa pole

By Jamhuri