………………………………………………………..

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiongozana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Dkt. Harrison Mwakyembe na Viongozi wa Chuo pamoja na wahitimu mbalimbali kuelekea katika Viwanja vya Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo tarehe 03 Desemba 2022 Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango amewatunuku vyeti wahitimu elfu moja mia tatu themanini na tisa(1,389) wa ngazi mbalimbali katika chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi (muhus) huku kati yao wahitimu wa kike wakiwa ni mia tano hamsini na tisa(559).

wahitimu mia tatu sabini(370) wametunikiwa stashahada ya juu katika fani mbalimbali za afya na Sayansi shirikishi, wahitimu mia tano tisini na nne(594) wamepata shahada ya kwanza, wahitimu mia tatu na themanin na sita(386) wamepata shahada ya uzamili, wahitimu thelathini na mbili(32) wametunikiwa digrii za uzamini za Utaalam na watahiniwa wengine saba (7) wametunikiwa shahada za uzamivu wa udaktari wa falsafa.

Aidha kuna wahitimu hamsini na tisa(59) wa program mpya kumi (10) za uzamini ambazo ni magonjwa ya damu na saratani za watoto, Ufumbuzi magonjwa ya fahamu kwa njia ya mionzi, Upasuaji wa watoto, Magonjwa mahututi,Mzunguko wa damu katika upasuaji wa Moyo, Uuguzi katika fani ya magonjwa ya moyo, Uuguzi wa magonjwa wa Figo, Uuguzi wa wagonjwa wa saratani, Afya ya Jamii-sayansi ya utelekezaji, na Uchumi na Sera za Afya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi na baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili mara baada ya kukamilika kwa Mahafali ya Chuo hicho yaliofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Desemba 2022.

Kwa upande wake Profesa Andrea Pembe wakati akisoma hotuba katika mahafali hayo amesema kwamba Idadi ya wanafunzi kutoka mataifa ya nje wanaokuja kusoma katika chuo cha muhimbili yameongezeka kwa asilimia 46.9 ukilinganisha na mwaka jana huku wanafunzi tisini na nne(94) kutoka nchi ishirini (20) wakichaguliwa kujiunga na Muhas mwaka huu huku akibainisha nchi hizo kuwa ni Botswana, Burundi , Cameroon, Comoro, DRC, Ghana, Rwanda, India, Kenya, Liberia, Malawi, Namibia, Uholanzi, Nigeria, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Ustwatini, Uganda , Yemen na Zambia.

Ameongeza kwamba Uongozi wa chuo hicho unaishuruku Serikali ya awamu ya Sita kwa kutuma fedha za matumizi mengineyo pamoja na kuwalipa kwa wakati fedha za makato mbalimbali wafanyakazi wa chuo hicho

By Jamhuri