Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) kwa kufuzu kuingia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Africa Cup of Nations 2024) itakayofanyika nchini Ivory Coast.

Ametoa pongezi hizo leo (Ijumaa, Septemba 8, 2023)  wakati akiahirisha Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bungeni jijini Dodoma.

Ili kufuzu michuano hiyo Tanzania ilihitaji kushinda au kutoka sare katika mechi za kundi lake.

“Ninayo furaha sana kuipongeza Taifa Stars kwa kufuzu michuano ya kuwania kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika baada ya kupambana na Timu ya Taifa ya Algeria huko nchini Algeria jana.”

Katika mechi hiyo Taifa Stars ilitoka suluhu na kuifanya ipate tiketi ya kuendelea na mashindano hayo. 

“Ninaipongeza sana timu yetu ya Taifa na kuitakia kila la heri katika mashindano yajayo.  Nami nitumie fursa hii kuwasihi Watanzania wenzangu tuendelee kuwaunga mkono ili wapate hamasa zaidi na kutuletea ushindi.”

By Jamhuri