Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 16, 2024 amewasili Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambapo atakagua athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi.

Pia Mheshimiwa Majaliwa atazungumza na wananchi waliothirika na mafuriko hayo.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa pia ataelekea Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani ambapo pia atakagua athari za mafuriko pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo ya Muhoro na Chimbi.

Please follow and like us:
Pin Share