Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makala amesikiliza kero za wananchi wa mji wa Mpanda kwa staili ya aina yake.

Makala ambaye anaongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi katika ziara ya mikoa sita iliyoanzia Katavi,alifungua “zahanati ndogo” ya kusikiliza kero za wananchi wa Mpanda.

Katika kusikiliza kero hizo, Makala alikaa pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri pamoja na wakuu wa idara za serikali.

“ Aise! nimependa sana utaratibu huu yaani unaelezea shida zako kwa faragha” alisema mwananchi mmoja Happy Mwakwaya .

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Nchimbi alisema utaratibu unaotumiwa na Makalla ni wa kisayansi.

“CCM inasikiliza kero za wananchi kisayansi” alisema Dk Nchimbi huku akishangiliwa.

By Jamhuri