Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri , kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa TAMISEMI, Mkapa House leo jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI jijini Dodoma.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI, Mkapa House jijini Dodoma leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Please follow and like us:
Pin Share