Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka watumishi wa umma kutimiza wajibu wao na kusisitiza kuwa hatokuwa tayari kuvumilia uzembe kwa mtumishi yeyote bila kujali yeye ni nani.

“Arusha mmenipokea vizuri sana ila tutageukana sio muda mrefu…mmenifurahia sana ila tutageukana muda si mrefu, sitajali wewe ni nani, ulipataje hicho cheo labda kwa kuhonga, rushwa au uganga lakini nitakula sahani moja na wewe…lazima kila mtu awajibike kwenye nafasi yake.

“Usije kufikiri aaaah huyu alikuwa mwenezi sasa katoka kwenye uenezi atakuja huku amepoa..ujue kuna watu wanasema aaah huyu sasa hivi atakuwa amejifunza, hakuna nilichojifunza zaidi ya kuwashughulikia wazembe na wavivu.

“Mimi hapa hata niwe mkuu wa mkoa siku moja tu inatosha lakini awepo mtu mmoja tu akijua kwamba kuna mwanaume alipita hapa kufanyakazi…Rais Samia oyeee!

“Kwa hiyo kila mtu kwenye nafasi yake kama ni mkuu wa wilaya shika wilaya yako vizuri, kama ni mkurugenzi ishike halmshauri yako kikamilifu, kama ni mkuu wa idara kwenye idara yako hapo…mambo ya kusema sijui ilikuaje …mmh hapana…”

“Mimi kaka yangu Mongella huwa anatumia akili nyingi kuwaza kwa sababu unakuta mwingine labda ni mkubwa kiumri au mdogo…lakini sasa mimi huwa muda sina…mimi nimewaambia mwanzoni tumechelewa…” amesema.

Makonda ameyasema hayo leo wakati akizugumza kwenye kikao kilichokutanisha wajumbe wa Kamati ya Siasa, viongozi wa taasisi na idara mbalimbali wa Serikali ndani ya Mkoa wa Arusha.

By Jamhuri