Katibu wa NEC,Itikadi , Uenezi na Mafunzo CCM , Paul Makonda amewataka wanasiasa kuacha tabia ya kumtofautisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli.

Kauli hiyo ameitoa  Mach 26,2024 jijini Dar es Salaam  wakati akizungumza katika mapokezi ya ndege ya abiria ya ATCL , Boeng B 737-9 Makonda amesema Rais Samia anapotimiza miaka mitatu ya uongozi wake madarakani, kuna kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kazi nzuri anayoifanya na heshima anayoipa CCM kwa uaminufu wake hawana sababu ya kutembea kifua mbele kwa uaminifu wake.

Amesema kuna kasumba ya ujinga unaoendelea wa kutaka kumtofautisha Dk. Samia Suluhu Hassan na Hayati Dk. John Magufuli.

“Huwezi kuwatengenisha hao watu na viongozi wetu wanafiki wanaotaka kujipendekeza kwa Rais Samia kila wakipata jukwaa wanataka kufanya kama wanataka kumfananisha Samia kama si sehemu ya Dk. Magufuli,”amesema.

Amesema akiwa msemaji wa Chama, kila anachokifanya Dk. Samia ndicho ambacho alikifanya Dk. Magufuli na walisimama katika taifa wakatafuta kura kwa pamoja.

“Huwezi kuwatenganishi ningetamani leo iwe ni siku ya mwisho ya unafiki wa viongozi na wanasiasa uchwara wanaopambana kuwatengenisha viongozi hawa,”amesema.