Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, uongozi wa wilaya katika picha ya kumbukumbu na wawakilishi wa watu wenye ulemavu waliokabidhiwa baiskeli za magurudumu

Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, amewaasa wanafunzi wasichana katika Shule za Msingi na sekondari kujiepusha kabisa na mambo yanayoweza kuathiri maendeleo yao kimasomo.

Mama Magufuli amesema mambo mengi ya Kisasa hususan ya mitandao yamekuwa yakitengua mawazo chanya ya wasichana, na kuwashawishi waishi maisha ya mtandao ambayo mengi yao si maisha halisi.

“Kwa hiyo binti zango elekezeni akili, maarifa na juhudi katika masomo na sio mambo mengine yanayoweza kuathiri maendeleo yenu kimasomo kama vile mambo ya mitandao ambayo mengi sio yenye kuonesha maisha halisi”, alisema Mama Magufuli leo Machi 18, 2023 nyumbani kwake Chato, Mkoa wa Geita.

Mjane huyu wa Hayati Dkt. Magufuli alikuwa akiongea machache baada ya kutoa misaada ya taulo za wasichana na Baiskeli za magurudumu kwa Shule tatu za Sekondari za Wasichana zilizomo wilayani Chato

Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa na Uongozi wa serikali ya wilaya na idare ya Elimu, ni sehemu ya maazimisho ya kumbukumbu ya maka miwili ya kilo cha Hayati Dkt. Magufuli

Shule zilizonufaika na Masada huo ni Sekondari za Wasichana za Janeth Magufuli, Zakhia Meghji na Jikombe.

Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Wasichana za Wilayani Chato za  Zakhia Meghji, Janeth Magufuli na Jikombe wakimsikiliza Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, wakati wa hafla hiyo leo.
Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akitoa msaada wa baiskeli za magurudumu kwa wawakilioshi wa wenye ulemavu wakati wa hafla hiyo leo.
Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Wasichana za Wilayani Chato za  Janeth Magufuli na Jikombe wakimkabidhi risala zao Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, wakati wa hafla hiyo leo
Wanafunzi wa Shule za Sekondari ya Wasichana ya Jikombe katika picha ya kumbukumbu Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, na viongozi wa wilaya ya Chato wakati wa hafla hiyo leo.
Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, uongozi wa wilaya katika picha ya kumbukumbu na Walimu wa shule za Janeth Magufuli, Zakhia Meghji na Jikombe