Biashara ni pamoja na hali ya kununua na kuuza kuzalisha mali na kuuza utaalamu wito na makubaliano ya kipekee yenye lengo  la kibiashara kwa nia ya kupata faida.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi  wa TRA Richard Kayombo amesema biashara ni shughuli yeyote ili inayofanya hivi sasa au iliyofanyika huko nyuma au itakayofanyika siku za baadaye.

 

Amesema kwa mujibu wa sera ya taifa mwaka 2003 ya kuendeleza wajasiriamali wadogo na wakati biashara zimegawanyika katika makundi manne kwa kuangalia vigezo vya idadi ya waajiriwa na mtaji uliopo kama ifuatavyo.

 

Amesema kuwa kuna biashara ndogo sana hii ina idadi ya waajiriwa mmoja hadi nne na  kiasi chake cha mtaji ni kuanzia  Sh 1 hadi Sh 5,000,000,  biashara ndogo yenye watu watano hadi 49 mtaji wake ni  ni Sh 5,000,000 hadi Sh 200,000,000

 

Biashara ya kati watu 50 hadi 99 mtaji unaanzia Sh 200,000,000 hadi Sh 800,000,000 na biashara kubwa watu 100 na zaidi zaidi mtaji unatakiwa kuwa zaidi ya Sh 800,000,000.

 

Amesema vigezo vingine vinatumika kwa upande wa Mamlaka ya Mapato katika kuweka madaraja ya walipa kodi kulingana na ukubwa  na  kiasi cha mauzo kwa mwaka au kiasi cha kodi kinacholipwa kwa mwaka.

Sheria ya Kodi

Kwa mfanyabiashara ambaye hajishughulishi  na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kwa namna moja au nyingine anaguswa zaidi na sheria tatu kuu za kodi.

 

Anazitaja sheria hizo kuwa ni Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ( VAT)  ya mwaka 1997  iwapo anastahili kusajiliwa sheria ya ushuru wa stempu ya mwaka 1972.

 

Sheria hizo tatu zinasimamiwa na Idara ya Mapato ya Ndani baada ya Uongozi wa TRA kuunganisha Idara ya Kodi ya Mapato na Idara ya Kodi ya Ongezeko la Thamani  kuanzia Julai 1, 2005  kwa upande wa Idara ya Walipa Kodi Wakubwa inaendelea na ukadiriaji na ukusanyaji wa kodi kwa walipa kodi wakubwa waliosajiliwa na idara hiyo.

Sheria ya kodi ya mapato

Amesema kodi ya mapato ni kodi itozwayo kwa mtu mwenye mapato yake yatokanayo na vyanzo mbalimbali vilivyoanishwa kwenye sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004.

 

Amesema mapato mengine ni yale yatozwayo  kwa mtu mwenye mapato yake yatokayo na vyanzo mbalimbali vilivyoanishwa kwenye sheria kodi ya mapato ya mwaka 2004.

 

Kayombo amesema mapato yatozwayo kodi ni yale yatokanayo na biashara yoyote kwa muda wowote inapofanyika ajira yoyote afanyayo mtu.

 

“Uwekezaji katika rasilimali kama nyumba viwanja shamba na hisa, yapo mapato mengine yanayotozwa kodi ya zuio kikamilifu kwa viwango maalumu kama vile malipo ya gawio kutoka  kwenye kampuni ambazo ni Mkazi wa Tanzania riba itokayo na maliasili,” amesema Kayombo.

Mapato yatokanayo na biashara

Kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato 2004 mapato yanataozwa kodi kutokana na biashara ni faida au ziada itokayao na biashara kwa mwaka hivyo mapato ya biashara yanajumuisha faida kutoka na mauzo ya rasilimali za biashara kama vile kuuza bidhaa za duka la lejaleja au jumla

 

Amesema malipo anayolipwa mfanyabiashara kwa masharti ya kufanya biashara au kutofanya biashara kulingana  na masharti anayotaka mtu mwingine.

 

Zawadi au takrima anazolipwa mfanyabiashara kutokana na shughuli zake za biashara kiasi cha mapato yanayohusu biashara ambayo vinginezo yangegeuka kuwa mapato ya uwekezaji katika rasilimali kwa mtu anayefanya biashara ya kupangisha nyumba.

 

“Ni taratibu zipi mtu anayeanza biashara anapaswa kuzifuata mtu anayeanza biashara anatakiwa afuate taratibu zote za maombi ya leseni kwa kujaza maombi inayopatikana na ofisi ya biashara ya jiji, manispaa, mji au ofisi ya halmshauri ya wilaya au Wizara ya Viwanda  na Biashara.

 

“Akikamilisha hatua hiyo na maombi yake kukubaliwa  afike ofisi ya TRA ya wilaya au mkoa ulio karibu nayo ambapo atatakiwa kujaza fomu ya maombi ya Namba ya Utamabulisho wa Malipakodi (TIN) namba hiyo ya utamabulisho hutolewa bure bila malipo yeyote,” amesema.

 

Amsema baada ya mfanyabiashara kujaza fomu ya TIN atatakiwa kuchukua alama za vidole kisha atapatiwa cheti cha utambulisho wa mlipa kodi na Kamishina wa TRA.

 

Amesema kitambulisho hicho atakitumia  kwa mambo mengine kama  kupata leseni ya biashara ya aina yeyote na mahali popote Tanzania.

 

Kusajili vyombo vya mto kama vile gari na pikipiki au kuhamisha umiliki wake kusajili  na VAT, kusajili au kubadilisha hati ya kumiliki  ardhi na nyumba.

 

Amesema  pia kitamsaidia kusajili kampuni, jina la biashara hakimiliki au alama ya biashara, kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi au kufanya biashara ya uwakala wa forodha, kupata zabuni ya serikali, taasisi za serikali, mabenki, taasisi za fedha vyama vya ushirika na vyombo vya umma.

 

Faida nyingeni ni pamoja na kupata namba ya utambulisho mfanyabishara atapaswa kujaza fomu za makadirio  ya awali ya kodi ya mapato kwa kuweka  makisio ya mapato na kodi inayopaswa kulipa na ataelekezwa tarehe ya kulipa kodi hiyo.

 

Kwa utaratibu wa TRA ili kuweka jalada la kodi litafunguliwa kwa ajili ya kuweka taarifa zake zote kama mahojiano kati ya mlipa kodi na ofisa kodi nakala za makadirio ya kodi kumbukumbu za malipo ya kodi ritani za mapato za kila mwaka na hesabu za mizania kama zipo nakala za barua kwenda au kutoka kwa mlipakodi.

 

“Ni muhimu kwa mlipakodi kukumbuka namba yake ya utambulisho kila anapokwenda ofisi za TRA kwa shughuli mbalimbali za ukadiriaji na kulipa namba hiyo itarahisisha kupatikana kwa jalada lake la kodi.

Viwango vya ulipaji kodi

Kayombo amesema kuwa kodi ya mapato inalipwa kulingana na mapato yanayopatikana kutoka kwenye biashara, mapato hayo yanatozwa kwa viwango na taratibu zinazotofautiana na kulingana na pato la mtu.

 

Amesema kwa mujibu wa sheria ya kodi  ya mapato na viwango vya  kodi anavyopaswa kulipa mfanyabiashara vimegwanyika mara tatu.

 

Anazitaja kuwa ni sehemu ya kwanza ni ya viwango vinavyohusu wafanyabaishara binafsi na wadogo ambapo mauzo yao hayazidi Sh 20,000,000 kwa mwaka sehemu hiyo hutozwa kodi kutegemeana na mauzo.

 

Sehemu ya pili ni viwango kwa wafanyabiashara binafsi wengine ambao viwango vyake vya kodi hutegemea faida inayopatikana na kulingana na kumbukumbu za biashara na hesabu za mizania zilizokaguliwa.

Amesema sehemu ya tatu ni kwa upande wa kampuni mshirika, vilabu, ushirika na taasisi zingine ambapo kiwango maalumu hutozwa kwenye faida.

 

Hata hivyo Kayombo amesema kuwa viwango vya kodi huweza kubadilika kutegemea na mabadiliko katika sheria ya fedha inayosomwa kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka.

Utaratibu wakulipa kodi

Kayombo amesema kodi ya mapato inalipwa kwa utaratibu uliopangwa kwa mujibu wa sheria ulipaji wa kodi kwa awamu.

 

Amesema  mfanyabiashara anaruhusiwa kulipa kodi itokanayo na makisio yake ya mwaka kwa awamu nne yaani mwezi Machi Juni Septemba na Desemba kama kufunga hesabu za biashara kufuatana na mwaka wa kalenda.

Hata hivyo amesema kuwa iwapo kodi inayotakiwa kulipwa haizidi Sh 100,000 au kodi ya awamu moja haizidi Sh 25,000 kodi hiyo itaweza kulipwa yote mara moja.

 

Ulipaji wakodi ya mwisho wa mwaka

Baada ya kulipa kodi katika wamu nne na baada ya kufunga hesabu za mwaka kunakuwa  na kodi ambayo ni mwisho mara nyingi kiasi cha kodi hiyo sio kikbwa kama makadirio ya kodi za mkupuo yaliafanyika kwa uashihi.

Amesema kuwa kodi hiyo hulipwa  kwa mkupuo mmoja miezi sita baada ya mwaka wa mapato kuisha wakati wa kuwasilisha ritani na hesabu mizania.

 

Amesema walipa kodi wanashauriwa kuwa waangalifu sana wanapojikadiria mpato ya kodi ya awali ya kulipa kwa mujibu wa sheria inayotakiwa isiwe pungufu  ya asilimia 80 ya kodi halisi ambayo anastahili kulipwa.


 

4547 Total Views 2 Views Today
||||| 2 I Like It! |||||
Sambaza!