Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema vituo vya Polisi vya Wilaya ya Ikungi na Mkalama Mkoani Singida ambavyo vilikwama ujenzi wake tangu mwaka 2015 sasa vitaanza kujengwa muda wowote kuanzia sasa.

Waziri Masauni amesema hayo baada ya kuvikagua vituo hivyo alipofanya ziara ya siku moja mkoani humo, na kuwaambia waandishi wa habari kuwa ujenzi wa vituo hivyo utaanza mara moja kwa kuwa bajeti ya ujenzi wa vituo hivyo ilishatengwa katika mwaka huu wa fedha.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na askari na maafisa Polisi wa Kituo cha Polisi Nduguti, Wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara Mkoani humo, leo, kwa ajili ya kukagua ujenzi wa vituo vya Polisi Mkalama na Ikungi. Serikali imetenga Shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Ikungi, na Shilingi milioni 476 Kituo cha Polisi Mkalama Mkoani humo.. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ambaye alifanya ziara mkoani humo naye alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani kutoa majibu kwa kusimama kwa ujenzi wa vituo hivyo.

Waziri Masauni ambaye aliwasilia Mkoani humo alisema kuwa serikali inaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa Polisi ili wananchi nchini wapate huduma karibu na maeneno yao, hivyo katika bajeti ya mwaka huu wa fedha Serikali imetenga Bilioni 1.1 kukamilisha kituo cha Polisi Ikungi na Milioni 476 kwajili ya Kituo cha Polisi Mkalama.

“Serikali ya Rais Samia imeendelea kuboresha Mazingira ya Polisi ambayo yanaonekana kuwa duni kupitia mradi wa kujenga vituo vya Polisi nchini, tayari katika bajeti ya mwaka huu tumetenga Bilioni 1.1 kwajili kukamilisha Kituo cha Polisi Ikungi na Milioni 476 kwaajili ya Kituo cha Polisi Mkalama” Alisema Mhandisi Masauni,” alisema Masauni.

Mhandisi Masauni amesema ujenzi wa vituo vya Polisi vya Mkalama na Ikungi utafanyika kwa awamu hivyo kufika kwake kwenye Wilaya hizo ni Utekelezaji wa Maagizo ya Katibu Mkuu Chongolo pamoja na kuangalia namna nzuri ya kumalizia ujenzi huo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na askari na maafisa polisi wa Kituo cha Polisi Nduguti, Wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida, wakati alipofanya ziara mkoani humo, leo, kwa ajili ya kukagua ujenzi wa vituo vya Polisi Mkalama na Ikungi. Serikali imetenga Shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Ikungi, na Shilingi milioni 476 Kituo cha Polisi Mkalama Mkoani humo.

Aidha, Mhandisi Masauni amewatoa hofu askari Polisi kuhusu miundombinu yao ambapo amemwakikishia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida kuwa hivi karibuni atarudi kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya Jeshi hilo la Polisi.

“Niwatoe hofu askari pamoja na wananchi tunajua mazingira bado sio rafiki lakini kwa kuwa tumeshaanza kulifanyia kazi na kwamba ujenzi utakamilika katika muda uliopangwa” aliongeza Mhandisi Masauni.

Waziri Masauni amemaliza ziara yake ya siku moja mkoani humo ambapo aliambatana na viongozi wa wilaya zote pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoani humo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akitoka Kituo cha Polisi Nduguti, Wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida, kufanya ukaguzi wakati wa ziara yake Wilayani humo, leo. Serikali imetenga Shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Ikungi, na Shilingi milioni 476 Kituo cha Polisi Mkalama Mkoani humo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Stella Mutabihirwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson, wakati alipokuwa anatoka kukagua jengo la Kituo vha Polisi Ikungi mkoani Singida ambalo limesimama ujenzi kwa zaidi ya miaka saba, wakati alipofanya ziara ya kukagua kituo hicho pamoja na cha Wilaya ya Mkalama Mkoani humo, leo. Serikali imetenga Shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Ikungi, na Shilingi milioni 476 Kituo cha Polisi Mkalama Mkoani humo. 

By Jamhuri