Jana jioni kwenye mitandao ya kijamii ilizuka taarifa kuwa Masoud Kipanya amekamatwa na Jeshi la Kanda maalum Dar es Salaam kutokana na kati ya michoro yake ya katuni ikionekana kama inaigombanisha Serikali na Wananchi,
hata hivyo kituo cha Redio Clouds FM kilipomtamfuta Kamanda wa Mkoa, Razalo Mambosasa kudhibitsha juu ya taarifa hizo, alisema hana taarifa na hajui kama kweli amekamatwa kituo na kuwataka watoa taarifa wajitokeze kutoa taarifa za kituo gani alikamatwa.


Baada muda mfupi jana jioni kwenye ukurasa wake wa Twitter alijitokeza na kuandika maneno haya “Poleni kwa usumbufu na asanteni kwa kujali hali za wengine. Niko salama Alhamdulillah. Namshukuru pia aliyesambaza taarifa. ‘AMESAIDIA’.”

Licha ya Masoud Kipanya kueleza kwamba yeye ni mzima, na kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano wao, lakini hajasema alipokuwa kama ni kweli alikuwa amekamatwa na polisi, au nini hasa kilitokea.

Please follow and like us:
Pin Share