Watu 18 wameuawa akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine katika ajali ya helikopta iliyotokea nje ya Mji Mkuu wa Kyiv leo.

Taarifa ya Mkuu wa Polisi Ukraine, Ihor Klymenko imesema kati ya watu hao waliopoteza maisha wawili ni watoto, tisa kati ya waliouawa walikuwa ndani ya helikopta ya huduma za dharura.

Taarifa hiyo imesema helikopta hiyo ilianguka kando ya shule ya chekechea katika kitongoji cha mashariki mwa mji mkuu Kyiv
wakati helikopta hiyo iliposhuka katika kitongoji cha Brovary.

Kwa mujibu wa Klymenko waliopoteza maisha ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Denys Monastyrskyi, Naibu wake Yevhen Yenin na Katibu wa Jimbo la Wizara ya Mambo ya Ndani, Yurii Lubkovych na wengine.
Waziri, Denys Monastyrskiy, alikuwa na watu wengine wanane kwenye helikopta hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa kulikuwa na giza na ukungu wakati wa ajali hiyo na ripoti za awali zinasema helikopta hiyo iligonga shule ya chekechea kabla ya kuanguka karibu na jengo la makazi.

By Jamhuri